Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Pombe Humfanya Mtu kuwa Mtumwa

    Kiu ya mvinyo inapoendekezwa mtu kwa hiari yake mwenyewe huwekea mdomoni mwake funda ambayo humshusha chini katika hali iliyo mbaya kuliko ile ya mnyama, mtu ambaye alifanywa kwa sura ya Mungu. Akili hupumbazwa, na kupoozeshwa, tamaa mbaya za kinyama huamshwa, ndipo hufuata uhalifu wa sheria wenye kuishusha sana tabia. 83T 56I;KN 119.4

    Kwa mvuto wa kinywaji wanywacho, watu huongozwa kutenda mambo ambayo, kama wasingalikuwa wameonja kitu chenye kulevya na kurusha akili, wangeepuka kwa hofu kuyatenda. Wakiwa katika hali ya kulewa, wako kwenye mamlaka ya Shetani. Huwatawala, nao husaidiana naye. 9Te 24;KN 119.5

    Hivyo ndivyo (Shetani) atendavyo kazi akiwavuta watu kwa werevu kuziuza rono kwa pombe. Huutawala mwili, akili na roho, wala si mtu huyo tena, bali Shetani, ndiye ambaye hutenda mambo. Na ukatili wa Shetani hudhihirishwa kadiri mlevi auinuavyo mkono wake kumpiga mke ambaye ameahidi kumpenda na kumtunza siku zote za maisha yake. Matendo ya mlevi yanaonyesha ukali wa Shetani. 10MM 114;KN 119.6

    Watu wanaotumia pombe hujifanya wenyewe watumwa wa Shetani. Shetani huwashawishi wale ambao wana kazi za madaraka katika njia za magari ya moshi, meli, na wale walio wakuu wa mashua au motakaa zilizojaa watu kwenda kujifurahisha kwa anasa, kutimiza tamaa ya chakula iliyopotoka, na kwa kufanya hivi kumsahau Mungu na sheria zake.KN 120.1

    Hawawezi kuona kitu wanachokikaribia. Ishara hutolewa kwa makosa, na gari hugongana. Ndipo hufuata kushikwa na hofu kuu, mvunjiko na kufa. Hali ya mambo ya jinsi hii itazidi kuonekana. Maelekeo ya uharibifu wa mlevi hupitishwa kwa watoto wake, na kwa njia ya hao nao hata kwa vizazi vijavyo. 11Te 34, 38;KN 120.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents