Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Matokeo Yanayoletwa na Uchafu wa Tabia

  Wengine wafanyao maungamo makuu hawaifahamu dhambi ya mazoea mabaya na matokeo yake ya hakika. Mazoea yaliyokwisha kuimarika muda mrefu yameupofusha ufahamu wao. Hawatambui uovu mkubwa mno wa dhambi hii inayomwondolea mtu heshima, ambayo hudhoofisha mwili na kuharibu uwezo wa mishipa ya fahamu ubongoni. Kanuni inayoongoza tabia ya moyoni ni dhaifu mno haiwezi kushindana na mazoea yaliyokwisha kupata nguvu. Maneno mazito ya ujumbe utokao mbinguni hayawezi kuingia kwa nguvu katika moyo ambao haukujengewa boma la kuulinda na uzoefu wa kosa hili linalomwondolea mtu heshima. Mishipa hii ya fahamu ya ubongo imepotewa na afya yake kwa mambo mabaya ya kuiridhisha tamaa mbaya sana kwa anasa za mwili. 132T 347;KN 127.1

  Uasherati umefanya mengi zaidi ya uovu wo wote mwingine kuziharibu tabia za wanadamu. Unatendeka kwa kadiri kubwa ya kutisha nao huleta magonjwa karibu ya kila namna.KN 127.2

  Kwa kawaida wazazi hawadhani kuwa watoto wao hufahamu lo lote juu ya uovu huu. Mara nyingi wazazi ndio wenye dhambi hasa. Wametumia vibaya haki za ndoa yao, na kwa uzoefu wa kujifurahisha kwa anasa wameziimarisha tamaa zao mbaya za mwili yaani za ashiki. Na kadiri hizi zilivyoimarika, ndivyo tabia ya moyoni na uwelekevu vilivyodhoofika. Hali ya kiroho imeshindwa na tabia ya kinyama, wakiwa wanayo chapa ya tabia ya wazazi wenyewe. Watoto wanaozaliwa kwa wazazi hawa karibu siku zote watarithi mazoea haya ya kuchukiza ya uovu wa siri. Dhambi za wazazi hawa zitapatilizwa kwa watoto wao kwa sababu wazazi hawa wamewapa chapa ya tamaa mbaya walizo nazo wao wenyewe.KN 127.3

  Wale wanaoimarika kabisa katika dhambi hii inayoharibu mwili na roho hawawezi kupata raha ila kwa shida mpaka mzigo wao wa dhambi hii ya siri umefunuliwa kwa wale wanaoshirikiana nao. Udadisi huamshwa mara hiyo, na uvumi wa uovu huenezwa kutoka kijana mmoja hata kwa mwingine, na kutoka kwa mtoto mmoja hadi kwa mtoto mwingine, mpaka watu karibu wote wapate habari za tendo la dhambi hii yenye kumwondolea mtu heshima. 142T 391, 392KN 127.4

  Tendo la mazoea haya mabaya ya siri huharibu nguvu za uhai wa mwili. Matendo yote yasiyo lazima yenye kuzitumikisha nguvu za mwili mwishowe huleta ulegevu wa mwili. Miongoni mwa vijana kiungo kikuu cha uhai, ubongo, hutumikishwa vikali siku zao za ujana hata huwa na upungufu na uchovu mkubwa, na kuuacha mwili uweze kupatwa na magonjwa mengi ya namna nyingi malimbali kwa urahisi.KN 128.1

  Kama mtu akiwa na mazoea haya kutoka umri wa miaka kumi na mitano na kuendelea, mwili utakataa matumizi mabaya uliyoyapata, na unaoendelea kuyapata, nao utawafanya wapate adhabu ya uhalifu wa sheria zake, hasa kutoka umri wa miaka thelathini hadi thelathini na mitano, kwa maumivu mengi mwilini na magonjwa mbalimbali, kama vile ugonjwa wa ini na mapafu, maumivu ya neva, baridi yabisi, ugonjwa wa uti wa mgongo, ugonjwa wa figo, na kuwa na saratani. Baadhi ya mashine nzuri za mwili hushindwa, zikaacha kutenda kazi nzito zaidi itakiwayo kutendwa, ambayo huchafua utaratibu mzuri wa mwili na mara nyingi huwapo na ugonjwa mkali wa mwili, ghafula, na mwisho ni kufa.KN 128.2

  Kuyaangamiza maisha pole pole lakini kwa hakika namna hii ni dhambi kubwa machoni pa Mungu sawasawa na kumwua mtu ghafula. Watu wanaojiharibu wenyewe, kwa makosa, watapata adhabu hapa, na wasipotubu kwa kweli, hawataruhusiwa kuingia mbinguni baadaye kama vile mtu anayeua ghafula hataruhusiwa mbinguni. Mapenzi ya Mungu huthibitisha uhusiano uliopo baina ya asili ya ugonjwa na matokeo yake ya baadaye.KN 128.3

  Hatusemi kuwa vijana wote walio dhaifu ni wenye hatia ya haya mazoea mabaya. Kuna wale ambao wana moyo safi na bidii ya kufanya vyema yote yapasayo, ambao huumia kwa mambo mballmbali yanayowashinda.KN 128.4

  Uovu wa kisirisiri ni kitu kinachoharibu kusudi lililo bora, bidii, na nguvu za nia kufanya tabia njema ya dini. Wote ambao wana ujuzi wa kweli wa kile kinachotokana na kuwa Mkristo wanajua kwamba wafuasi wa Kristo wanao wajibu mkubwa kama wanafunzi wake kuzitiisha tamaa zao zote, uwezo wao wote wa mwili na uelekevu wa akili zao chini ya mapenzi yake. Wale wanaotawaliwa na tamaa zao mbaya hawawezi kuwa wafuasi wa Kristo. Wamejitoa sana kumtumikia bwana wao, yaani, mwanzishaji wa kila ovu, hata hawawezi kuyaacha mazoea yao mabaya na kuchagusa kumtumikia Kristo. 15CG 444., 446;KN 128.5

  Vijana wanapochagua mazoea mabaya sana wakati moyo ungali mwepesi kuumia, kamwe hawatapata nguvu za kukua kwa ukamilifu na kwa usawa wa mwili, akili, na tabia ya moyoni. 162T 351;KN 128.6

  Tumaini tu la wale wenye mazoea mabaya sana ni kuyaacha milele ikiwa wanaithamini afya hapa na wokovu wa milele baada ya maisha haya. Mazoea haya yanapoendekezwa kwa muda mrefu, inatakikana jitihada kubwa kuyapinga na kukataa kujifurahisha kwa anasa mbaya. 17 CG 464;KN 128.7

  Usalama tu kamili kwa watoto wetu juu ya kila tendo la upotovu ni kutafuta kukubaliwa kuingia zizini mwa Kristo na kuwekwa chini ya ulinzi wa Mchungaji mwaminifu na wa kweli. Yeye atawaokoa na kila ovu, na kuwakinga wasipatwe na hatari yo yote, kama wataitii sauti yake. Asema, “Kondoo wangu waisikia sautiKN 129.1

  yangu na wanifuata.” Ndani ya Kristo watapata malisho, nguvu, na tumaini; hawatasumbuliwa na tamaa zisizotulia za kutaka kitu kuzipotosha akili na kuuridhisha moyo. Wameiona lulu ya thamani kuu, na moyo umetulia na kupata raha. Furaha yao ni ya namna safi, ya amani, bora, ya mbinguni. Hawayaruhusu masingizio, wala majuto. Furaha za namna hii hazidhuru afya wala kulegeza nguvu za akili, bali ni zenye kutia afya. 18 CG 467KN 129.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents