Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya 18 - Kuchagua Mume au Mke

    NDOA ni jambo ambalo litakuwa na mvuto na matokeo katika maisha yako ulimwengungi humu na katika ulimwengu ujao pia. Mkristo mwaminifu hataendelea na mipango yake katika jambo hili pasipo kufahamu kuwa Mungu anaikubali njia yake. Hatataka Kujichagulia. Haitupasi kujipendeza wenyewe, kwa maana Kristo hakujipendeza mwenyewe. Maana yangu siyo kwamba mtu awaye yote angeoana na mtu asiyempenda. Hiyo ingekuwa dhambi. Lakini mahaba na hali ya kuvutwa kwa urahisi visiruhusiwe kuleta uharibifu. Mungu ataka moyo wote, upendo halisi.KN 130.1

    Wale wanaonuia kuoana ingewapasa kufikiri namna ya tabia na mvuto wa nyumba wanayotaka kuianzisha . Wanapokuwa wazazi, ndipo wanakabidhiwa kazi takatifu. Hali njema ya watoto wao katika maisha haya na raha ya maisha yajayo huwategemea wazazi zaidi. Kwa kadiri kubwa, wazazi ndio wanaokaza tabia za kiroho na za kimwili pia ambazo watoto huzifuatisha. Hali ya mtaani inategemea hali ya nyumba moja moja za watu wanaoishi pale. Mvuto wa kila nyumba utasaidia kuinua hali ya jamii ya watu mtaani ama kuishusha hadhi yake.KN 130.2

    Yawapasa vijana Wakristo kutumia uangalifu mwingi katika kufanya urafiki na katika kuchagua wachumba. Angalia isiwe kile unachokidhania sasa kuwa dhahabu safi kikatokea kuwa madini nyingine isiyo dhahabu. Marafiki wa kidunia huelekea kuweka vikwazo katika njia ya kazi yako kwa Mungu, na roho za wengi huharibiwa na urafiki usio mzuri wala furaha, ama kazini ama ndoani, na wale ambao kamwe hawawezi kuinua hali au kuadilisha.KN 130.3

    Pima kila jambo na kuangalia maendeleo yote ya tabia ya yule ambaye wafikiri kuungana naye katika maisha yako yote. Hatua unayokaribia kufanya ni moja iliyo ya maana sana maishani mwako, na isingefanyawa kwa haraka. Huku ukiwa na upendo. Angalia usikupofushe macho.KN 130.4

    Chunguza kwa uangalifu ili kuona kama maisha yako va ndoa yatakuwa ya furaha au ya kutokupatana na mabaya. Hebu jiulize, Umoja huu utanisaidia kuelekea mbinguni? Utaniongezea upendo wangu kwa Mungu? Tena utazidisha ukubwa wa manufaa yangu katika maisha haya? Kama mawazo haya hayana kizuizi, basi, kwa kicho cha Mungu songa mbele.KN 130.5

    Kuchagua mchumba kungekuwa sawa kabisa na kutafuta kujipatia hali bora ya mwili akili, na moyo kwa ajili ya wazazi kwa ajili ya watoto wao; hali ambayo itawawezesha wazazi na watoto kuwanufaisha wanadamu wenzao na kumtukuza Mwumbaji wao.KN 130.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents