Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya 21 - Masikilizano na Maisha ya Heri

    MUNGU ameamuru kwamba yapasa pawepo upendo kamili na masikilizano kati ya wale wanaofunga ndoa na kuoana. Bibi arusi na bwana arusi, mbele za wote mbinguni na duniani, wamepaswa kuahidi kupendana kama Mungu alivyowaamuru. Ni wajibu wa mke kumstahi na kumheshimu mumewe, na ni juu ya mume kumpenda na kumfurahia mkewe.KN 148.1

    Wanaume na wanawake, mwanzoni mwa maisha yao ya unyumba, wangejitoa wakfu kwa Mungu.KN 148.2

    Ingawa ndoa imepangwa kwa uangalifu na busara namna gani, ni watu wachache sana ambao huwa wameungana kabisa moyoni wakati ibada ya ndoa inapofanywa. Umoja wa kweli wa wale wawili wenye kuoana ni kazi ya miaka ifuatayo.KN 148.3

    Mashaka na masumbufu ya maisha yanapoanza kuwapata wale waliooana karibuni, ile hali ya mahali iliyodhaniwa juu ya ndoa huanza kupungua. Mume na mke huanza kujifunza tabia zao wao kwa wao jinsi ambavyo hawakuweza kujuana zamani. Huu ndio wakati wa hatari sana katika maisha yao. Raha na utumizi wa maisha yao yote yafuatayo hutegemea kama wanavyoendeleza mwenendo wao mwema wakati huu. Mara nyingi watagundua katika tabia zao wao kwa wao manyonge na makosa fulani ambayo hawakuyashuku zamani; lakini pia mioyo ambayo imeungwa na upendo itagundua sifa zilizo bora zisizojulikana zamani. Basi, wote na watafute mema kuliko kutafuta mawaa. Mara nyingi ni mafikira yetu wenyewe, hali ya roho zetu sisi wenyewe, ambazo zinayakinisha mambo tutakayoyagundua kwa mwingine.KN 148.4

    Kuna wengi ambao kufikiri ya kwamba kudhihirisha upendo ni kama kujipotezea hadhi, nao hukaa katika hali ya unyamavu unaowazuia wengine. Moyo wa namna hii huzuia mtu asidhihirishe huruma yake. Nguvu za wema na upaji zikizuiwa, hufifia, na moyo hubaki hali ya upweke na kupooza. Inatupasa kujihadhari na kosa hili. Upendo hauwezi kuaumu sana kama usipodhihirishwa. Usiache nata mmojawapo wa nyumba yako afadhaike moyoni kwa kutamani upendo na huruma yako, asipate.KN 148.5

    Kila mmoja na aonyeshe upendo kuliko kuulazimisha. Kuzeni mambo yaliyo bora katika maisha yenu, na kuwa wepesi kwa kutambua sifa njema ninyi kwa ninyi. Kujua kwamba umethaminiwa na mwenzako ni jambo litialo nguvu na kuridhisha moyo Huruma na staha humtia kila mmoja nguvu apata kuwa bora zaidi, na upendo wao kwa wao huzidishwa kwa vile unavyowatamanisha wazidi kuwa watu wenye makusudi mema.KN 148.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents