Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Ujumbe Watolewa na Watu Duni

    Kama wanateolojia wangekuwa walinzi waaminifu, wenye bidii na kwa maombi wakiyachunguza Maandiko Matakatifu, wangekuwa wameutambua wakati. Unabii ungewafunulia matukio ambayo yamekaribia kutimia. Lakini ujumbe ulihubiriwa na watu wanyenyekevu,. Wale wanaopuuzia kuutafuta ukweli ikiwa wanaweza kuupata wameachwa gizani. Lakini Mwokozi anasema, “yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.” Yohana 8:12. Kwa mtu huyo baadhi ya nyota zenye mng’ao wa mbinguni zitatumwa kumwongoza katika nuru yote.TK 200.3

    Wakati Kristo alipokuja mara ya kwanza makuhani na waandishi wa Mji Mtakatifu wangezielewa “dalili za nyakati” na kutangaza ujio wa yeye aliyeahidiwa. Mika alieleza siku yake ya kuzaliwa. Danieli alieleza habari za kuja kwake mara ya kwanza. Mika 5:2, Danieli 9:25. Viongozi wa Wayahudi hawakuwa na kisingizio chochote iwapo walikuwa hawajui. Kutokujua kwao ilikuwa ni matokeo ya dhambi na kiburi cha kutojali.TK 200.4

    Kwa ufahamu mkubwa wazee wa Israeli wangepaswa kujifunza mahali, wakati, mazingira, ya tukio kubwa la historia ya ulimwengu kuja kwa Mwana wa Mungu. Watu walitakiwa wawe wanakesha ili waweze kumkaribisha Mkombozi wa ulimwengu. Lakini kule Bethlehemu wasafiri wawili walikuwa wamechoka kutoka Nazareti walipita katika njia ndefu ya mtaani iliyo nyembamba ya kuelekea upande wa mashariki kabisa mwa mji, wakitafuta mahali pa kulala usiku bila mafanikio. Hakuna mlango uliofunguliwa ili kuwakaribisha. Katika banda bovu lililokuwa limeandaliwa kwa ajili ya ng’ombe hatimaye walipata mahali pa kimbilio la kujihifadhi, na hapo Mwokozi wa ulimwengu alizaliwaTK 201.1

    Malaika walipewa jukumu la kupeleka habari za furaha kwa wale waliokuwa wamejiandaa kuzipokea na ambao kwa furaha wangezieneza habari hizo. Kristo alinyenyekea akabeba asili ya mwanadamu, akabeba huzuni ili kuitoa nafsi yake kafara kwa ajili dhambi. Lakini malaika walitamani hata katika hali yake ya kudhalilishwa, Mwana wa Aliye juu angeonekana mbele za wanadamu akiwa na heshima na utukufu unaolingana na tabia yake. Je, watu wakuu wa dunia wangekusanyika katika mji mkuu wa Israeli kumpokea anapokuja. Je, malaika wangeandamana naye kwa kundi kubwa lililotarajiwa?TK 201.2

    Malaika alitembelea dunia kuwaona wale waliokuwa wamejiandaa kumkaribisha Yesu. Hakuisikia sauti ya kusifu kwamba wakati wa kuja kwa Mwokozi ulikuwa karibu. Malaika alizungukazunguka huku na huko juu ya mji mteule na hekalu ambamo uwepo wa Mungu ulidhihirika kwa vizazi vingi, hata hapo kulikuwa na kutojali kwa namna ileile. Makuhani walitoa kafara zenye unajisi kwa majivuno na kiburi. Mafarisayo, kwa sauti za kupayuka walikuwa wakiwahutubia watu na kutoa maombi ya kujisifu kwenye njiapanda za mitaa. Wafalme, wanafalsafa, walimu wa sheria, wote hawakuujali ukweli wa kustaajabisha kwamba Mwokozi wa wanadamu alikuwa karibu kuonekana.TK 201.3

    Kwa mshangao mjumbe wa mbinguni alitaka kurudi mbinguni akiwa na habari za kuaibisha, alipogundua kundi la wachungaji waliokuwa wakilinda mifugo yao. Kadiri walipoitazama kwa mshangao mbingu iliyokuwa imejaa nyota nyingi, waliuelewa unabii wa Masihi ajaye na walikuwa na hamu ya ujio wa Mkombozi wa ulimwengu. Hapa kulikuwa na kundi ambalo lilikuwa limeandaliwa kuupokea ujumbe wa mbinguni. Ghafla utukufu wa mbinguni ulitawala eneo lote, kundi la malaika wasioweza kuhesabika lilionekana; na kana kwamba haikutosha kwa mjumbe mmoja kuleta furaha iliyokuwa kuu sana kutoka mbinguni, sauti nyingi zilisikika katika wimbo ambao mataifa yote ya waliokombolewa wataimba siku moja: “Atukuzwe Mungu juu mbinguni, Na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia.” Luka 2:14.TK 201.4

    Ni somo zuri sana la kisa hiki cha ajabu cha Bethlehemu! Jinsi kinavyokemea kutokuamini kwetu, kiburi na hali ya kuridhika tuliyonayo. Jinsi kisa hiki kinavyotutahadharisha kuwa waangalifu, ili sisi pia tusije tukashindwa kuzitambua ishara za nyakati na kwa hiyo tukashindwa kuijua siku ya kujiliwa kwetu.TK 202.1

    Sio tu miongoni mwa wachungaji wanyenyekevu ambapo malaika waliwakuta watu wanaosubiria ujio wa Masihi. Kwa watu wa mataifa pia walikuwepo watu waliokuwa wanatazamia ujio wa Masihi-watu matajiri na wenye hekima-wanafalsafa kutoka Mashariki. Katika Maandiko ya Kiebrania watu hawa walikuwa wanajifunza habari za nyota itakayoinuka katika Yakobo. Kwa shauku kubwa waliusubiria ujio wake Yeye ambaye hatakuwa tu “faraja ya Israeli” bali “Nuru ya kuwaangazia mataifa” na kuwa wokovu hata mwisho wa dunia.” Luka 2:25, 32; Matendo 13:47. Nyota ya mbinguni iliyotumwa iliwaongoza wageni kutoka mataifa ya mbali hadi kwenye sehemu aliyozaliwa mfalme wa dunia.TK 202.2

    Ni kwa “Wale wamtazamiao kwa wokovu” ndio ambao Kristo “atatokea mara ya pili, pasipo dhambi” Waebrania 9: 28. Kama habari za kuzaliwa kwa Mwokozi, ujumbe wa kuja kwa Kristo haukukabidhiwa kwa viongozi wa kidini. Waliikataa nuru kutoka mbinguni; kwa hiyo wao hawakuwemo katika idadi aliyoeleza mtume Paulo: “Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi.TK 202.3

    Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi sio wa usiku, wala wa giza.” 1 Wathesalonike 5: 4, 5.TK 202.4

    Iliwapasa walinzi kwenye kuta za Sayuni kuwa wa kwanza kuzipata habari za ujio wa Mwokozi, iliwapasa wawe wa kwanza kutangaza kwamba yuko karibu. Lakini walikuwa wamekaa tu pasipo jitihada yoyote wakati watu wakiwa wamelala katika dhambi zao. Yesu aliliona kanisa lake, kama mtini usiozaa uliofunikwa na majani yadanganyayo wakati haukuwa na matunda. Roho ya unyenyekevu wa kweli, toba na imani vilikosekana. Kulikuwa na kiburi, dini ya matendo, ubinafsi, ukandamizaji. Kanisa lililorudi nyuma lilifumbia macho ishara za nyakati. Walimwacha Mungu na kujitenga na upendo wake. Kadiri walivyopuuzia kuishi sawasawa na maagizo, ahadi yake haikutimizwa kwao.TK 203.1

    Wengi miongoni mwa wale waliodai kuwa wafuasi Wakristo walikataa kuipokea nuru kutoka mbinguni. Kama walivyokuwa Wayahudi wa zamani, hawakuujua wakati wa kujiliwa kwao. Bwana aliwapita wao na akawafunulia ukweli wake watu ambao kama walivyokuwa wafugaji wa Bethlehemu na mamajusi wa Mashariki, walizingatia ukweli wote waliokuwa wameupokea.TK 203.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents