Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya 2 - Wakristo Wa Awali-Watii Na Wakweli

    Yesu aliwaeleza wanafunzi wake mambo ambayo watu wake wangeyapitia tangu alipotwaliwa kutoka kwao, hadi atakaporudi katika nguvu na utukufu. Alipokuwa akitazama ndani kabisa katika wakati ujao, jicho lake liliona dhoruba kali ambazo zingewakumba wafuasi wake katika nyakati za mateso zilizokuwa zinakuja. Soma Mt. 24:9, 21, 22. Iliwapasa wafuasi Wakristo kupita katika njia ile ile ya kukataliwa na mateso ambayo Bwana wao aliipitia. Uadui dhidi ya Mkombozi ungedhihirishwa kwa wote ambao wangeliamini jina lake.TK 30.1

    Upagani uliona kwamba kama Injili ingeshinda, mahekalu na madhabahu zake zingefutiliwa mbali; kwa hiyo, moto wa mateso ukawashwa. Wakristo wakanyang’anywa mali zao na kutolewa katika nyumba zao. Watu wengi, waungwana na watumwa, matajiri na maskini, wenye elimu na wasio na elimu, wakauawa bila huruma.TK 30.2

    Tangu wakati wa Nero, mateso yaliendelea kwa kame kadhaa. Wakristo walisingiziwa kuwa vyanzo vya njaa, maafa na matetemeko. Watoa habari walikaa tayari kulipwa kwa kuwasaliti hawa ambao hawakuwa na hatia kwa kusema kuwa ni waasi na wasumbufu katika jamii. Wengi walitupwa mbele ya wanyama mwitu na kuchomwa wakiwa hai katika matanuru. Baadhi walisulubishwa; wengine wakafunikwa na ngozi za wanyama wa porini na kutupwa katika viwanja vya maonesho ili wararuliwe na mbwa. Katika matukio ya sherehe, umati mkubwa wa watu ulikutana kufurahia maonesho hayo na walicheka na kushangilia vilio vya waliokuwa wakifa.TK 30.3

    Wafuasi Wakristo walilazimika kutafuta maficho katika sehemu zilizojitenga. Chini ya vilima nje ya mji wa Roma, mapango marefu yalichimbwa katika ardhi na miamba kwa kilometa nyingi nje ya kuta za mji. Ndani ya makimbilio haya ya chini ya ardhi, wafuasi Wakristo walizika wafu wao; huko ndiko walikopata makazi wakati wametengwa. Wengi waliyakumbuka maneno Bwana wao aliyowaambia, kwamba wakati watakapoteswa kwa ajili ya Kristo, wafurahi kabisa. Tuzo yao ni kubwa mbinguni, kwani ndivyo manabii walivyoteswa kabla yao. Soma Mt. 5:11, 12.TK 30.4

    Nyimbo za ushindi zilisikika kutoka katikati ya moto. Kwa imani walimwona Kristo na malaika wakiwaangalia kwa shauku kubwa na kuheshimu uthabiti wao na kuukubali. Sauti ilikuja toka katika kiti cha enzi cha Mungu: “Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.” Ufu. 2:10.TK 31.1

    Juhudi za Shetani kuangamiza kanisa la Kristo kwa vurugu hazikusaidia. Watendakazi wa Mungu waliuawa, lakini Injili ilizidi kuenea na wafuasi wake waliongezeka. Mkristo mmoja alisema: “Kadiri mnavyotufyeka, ndivyo tunavyoongezeka; damu ya Wakristo ni mbegu.” 2Tertullian, Apology, paragTK 31.2

    Kwa hiyo, Shetani aliweka mipango yake kupambana na Mungu kwa ufanisi zaidi kwa kupandisha bendera yake katika kanisa la Kikristo ili akipate kwa hila kile alichoshindwa kukipata kwa nguvu. Mateso yakakoma. Badala yake kukawa na vishawishi vya mafanikio na heshima ya kidunia. Waabudu sanamu walipewa kupokea sehemu ya imani ya Kikristo, wakati wakiukataa ukweli muhimu. Walidai kuwa wamempokea Kristo lakini walikuwa hawajashawishika kuwa ni wenye dhambi na hawakuwa wanaona haja ya toba wala badiliko la moyo.TK 31.3

    Sasa kanisa lilikuwa katika hatari ya kutisha. Jela, mateso, moto na upanga vilikuwa baraka ukilinganisha na jambo hili! Baadhi ya Wakristo walisimama imara. Baadhi walikubali kubadili imani yao. Akiwa na vazi la ukristo wa bandia, Shetani alijipenyeza kanisani na kupotosha imani yao.TK 31.4

    Hatimaye, Wakristo wengi walikubali kushusha kiwango. Ukaundwa umoja kati ya Ukristo na upagani. Ingawa waabudu sanamu walidai kuwa wamejiunga na kanisa, bado waliendelea kung’ang’ania ibada zao za sanamu, wakibadilisha tu vitu walivyokuwa wakiviabudu kuwa sanamu za Yesu, Mariamu na hata watakatifu wengine. Mafundisho yasiyokubalika, kanuni za kishirikina, na sherehe za ibada ya sanamu zikaingizwa katika imani na ibada za kanisa. Kanisa la Kikristo likapotoshwa, na kupoteza usafi na nguvu yake. Hata hivyo, baadhi hawakupotoka. Waliendelea kuwa waminifu kwa yule aliye chanzo cha ukweli.TK 31.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents