Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kukata Tamaa Hadi Uhakika

    Wanafunzi walikuwa wamemwona “Yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati na manabii,” (Yohana 1:45) kwa ukamilifu zaidi kuliko pale mwanzo. Mashaka, na kukata tamaa, vilitoa nafasi kwa matumaini, na imani safi. Walikuwa wamepita katika majaribu makali kuliko yote waliyokuwa wanaweza kuyapitia, na walikuwa wameona jinsi neno la Mungu lilivyotimizwa kwa ushindi. Baada ya hapo hakuna jambo ambalo lingeweza kutishia imani yao? Katika huzuni kuu waliyokuwa nayo, walipata “faraja iliyo imara,” yaani, tumaini lilikuwa kama “nanga ya roho yenye salama, yenye nguvu.” Waebrania 6:18,19.TK 222.2

    Bwana asema: “Watu wangu hawatatahayari kamwe.” “Kilio huja usiku, lakini asubuhi huwa furaha.” Yoeli 2:26; Zaburi 30:5. Siku ya kufufuka kwake, wanafunzi hawa walikutana na Mwokozi, na mioyo yao iliwaka ndani yao kadiri walivyokuwa wakisikiliza maneno yake. Kabla ya kupaa kwake, Yesu aliwaagiza, “Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe,” kisha akasisitiza, “Tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote.” Marko 16:15; Mathayo 28:20. Katika siku ya Pentekoste Mfariji aliyekuwa ameahidiwa alishuka, na mioyo ya waumini iliburudika kwa kutambua uwepo wa Bwana wao aliyekuwa amepaa.TK 222.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents