Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kuungana na Ulimwengu

    Makanisa mengi ya Kiprotestanti yamefuata nyayo za Kanisa la Roma kwa kushikamana na “wafalme wa dunia”—yaani, makanisa ya kitaifa, kwa kushikamana na serikali za kidunia; na madhehebu mengine, kwa kutaka kupendwa na ulimwenguni. Neno “Babeli” (au, machafuko) linaweza kuwakilisha taasisi hizi zinazodai kuwa zinatoa mafundisho katika Biblia, lakini zimegawanyika katika madhehebu nyingi zenye mafundisho yanayopingana.TK 243.2

    Kitabu kimoja cha Kikatoliki kinasema kwamba “kama Kanisa la Roma lina hatia ya ibada ya sanamu kwa sababu ya watakatifu; binti yake Kanisa la Uingereza, ana hatia hiyo hiyo kwani ana makanisa kumi yaliyopewa heshima ya Mariamu kwa kila kanisa moja lililopewa heshima ya Kristo.” 217Richard Challoner, The Catholic Christian Instructed, Preface, pp. 21, 22.TK 243.3

    Naye Dk. Hopkins anasema: “Hakuna sababu ya kudhania kuwa tabia na desturi za upinga Kristo zinahusu kanisa ambalo leo linaitwa Kanisa la Roma. Makanisa ya Kiprotestanti yana upinga Kristo mwingi, na bado hayajabadilika ipasavyo ... kutoka katika ufisadi na uovu.” 218Samuel Hopkins, “A Treatise on the Millennium,” Works, vol. 2, p. 328.TK 243.4

    Kuhusu Kanisa la Presbyterian kujitenga na Kanisa la Roma, Dk. Guthrie aliandika: “Miaka mia tatu iliyopita, kanisa letu, likiwa na Biblia iliyo wazi katika nembo yake, na mwito usemao “Yachunguzeni Maandiko” katika bango lake, lilitoka katika malango ya Roma.” Kisha aliuliza swali muhimu: “Je walitoka Babeli wakiwa safi?” 219Thomas Gruthrie, The Gospel in Ezekiel, p. 237.TK 243.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents