Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Jambo Halisi Mbinguni

    Jambo lililokuwa linafanyika kama kielelezo katika huduma ya patakatifu pa duniani, linafanyika kikweli katika patakatifu pa mbinguni. Baada ya kupaa kwake, Mwokozi wetu alianza kazi kama kuhani wetu mkuu: “Kwa sababUkristo hakuingia katika patakatifu palipofanyika kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu halisi; bali aliingia mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu.” Waebrania 9:24.TK 263.1

    Huduma ya kuhani katika chumba cha kwanza, “ndani ya pazia” lililokuwa linatenganisha patakatifu na ua wa nje, inawakilisha kazi ambayo Kristo aliianza baada ya kupaa. Katika huduma ya kila siku kuhani alikuwa anawasilisha mbele ya Mungu damu ya ile sadaka ya dhambi, na pia uvumba ambao ulipanda pamoja na maombi ya Israeli. Ndivyo Kristo alivyosihi kwa damu yake mbele ya Baba kwa niaba ya wenye dhambi na kuwasilisha mbele yake, maombi ya wenye dhambi waliotubu pamoja na harufu nzuri ya haki yake. Hivyo ndivyo huduma ilivyokuwa katika chumba cha kwanza cha patakatifu pa mbinguni.TK 263.2

    Huko ndiko imani ya wanafunzi wa Yesu ilikomfuata wakati amepaa. Hapo ndipo matumaini yao yalipokuwa, “matumaini ... tuliyo nayo kama nanga ya roho, yenye salama, yenye nguvu, yaingiayo hata mle mlimo ndani ya pazia, alimoingia Yesu kwa ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa kuhani mkuu hata milele.” “Kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele.” Waebrania 6:18-19, 20; 9:12.TK 263.3

    Kazi hii iliendelea katika chumba cha kwanza cha patakatifu kwa kame kumi nane. Damu ya Kristo ilileta msamaha na kukubalika mbele za Baba kwa niaba ya waumini waliotubu, lakini dhambi zao zilibaki katika vitabu vya kumbukumbu. Kama ilivyokuwa katika huduma kielelezo, kulikuwa na kazi ya upatanisho mwishoni mwa kila mwaka, vivyo hivyo kabla ya kazi ya Kristo kwa ajili ya wanadamu kukamilika, kuna kazi ya upatanisho kwa ajili ya kuondoa dhambi kutoka patakatifu. Kazi hii ilianza mwishoni mwa zile siku 2300. Wakati huo Kuhani Mkuu aliingia patakatifu sana kupatakasa patakatifu.TK 263.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents