Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya 24 - Yesu Anafanya Nini Sasa?

    Suala la patakatifu lilifumbua lile fumbo la kuvunjika kwa matumaini. Liliweka wazi mfumo mzima wa ukweli mwingi, uliokuwa unahusiana na kupatana, kuonesha kuwa mkono wa Mungu ulikuwa umeongoza zile harakati za Ujio. Wale waliokuwa wametazamia Ujio wa pili kwa imani walikuwa wanamtegemea atokee katika utukufu, lakini matumaini yao yalipovunjika, wakawa hawanwoni Yesu. Sasa walikuwa wakimtazama Kuhani wao Mkuu tena katika patakatifu sana, ambaye anakuja upesi kama mfalme na mkombozi. Nuru kutoka patakatifu iliangazia mambo yaliyopita, yaliyopo, na yajayo. Ingawa walikuwa hawakuuelewa ujumbe waliokuwa wanautoa, bado ujumbe huo ulikuwa wa kweli.TK 265.1

    Kosa halikuwa katika kuhesabu vipindi vya unabii, lakini lilikuwa juu ya tukio ambalo lingetokea mwishoni mwa zile siku 2300. Hata hivyo yote yaliyokuwa yametabiriwa na unabii huo yalikuwa yametimia.TK 265.2

    Kristo alikuwa amekuja, lakini si duniani, bali patakatifu sana pa hekalu la mbinguni: “Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye.” Danieli 7:13.TK 265.3

    Ujio huu ulitabiriwa na Malaki: “Angalieni, namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu; naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu lake ghafula; naam, yule mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anakuja, asema Bwana wa majeshi.” Malaki 3:1. Ujio wa Bwana katika hekalu lake ulikuwa wa “ghafla” usiotarajiwa na watu wake. Walikuwa hawamtafuti hapo.TK 265.4

    Watu hawakuwa tayari kukutana na Bwana wao. Bado kulikuwa na kazi ya maandalizi juu yao. Wanapomfuata Kuhani wao Mkuu katika huduma yake, kazi mpya zitafunuliwa. Ujumbe mwingine ulikuwa unapasa kutolewa kwa kanisa.TK 265.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents