Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya 25 - Sheria Ya Mungu Haibadiliki

    “Kisha Hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na l\sanduku la agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake.” Ufunuo 11:19. Sanduku la agano la Mungu liko patakatifu pa patakatifu, yaani chumba cha pili cha patakatifu. Katika huduma za hema ya duniani, ambazo zilikuwa “mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni” (Waebrania. 8:5), chumba hiki kilifunguliwa katika siku ya upatanisho tu kwa ajili ya kupatakasa patakatifu. Kwa hiyo maneno yanayosema kwamba hekalu la Mungu lilifunguliwa mbinguni na sanduku la agano lake likaonekana, yanaonesha kufunguliwa kwa patakatifu pa patakatifu pa mbinguni mwaka 1844 wakati Kristo anaingia humo kufanya kazi ya mwisho ya upatanisho. Wale waliomfuata kwa imani Kuhani wao Mkuu alipokuwa anaingia patakatifu sana, waliliona sanduku la agano lake. Kadiri walivyokuwa wakilichunguza suala la patakatifu walilielewa badiliko la huduma ya Mwokozi, na waliona kwamba, sasa alikuwa anahudumu mbele ya sanduku la Mungu.TK 270.1

    Sanduku lililokuwa katika hema ya duniani lilikuwa na mbao mbili za mawe ambazo zilikuwa zimeandikwa sheria ya Mungu. Hekalu la Mungu lilipofunguliwa kule mbinguni, sanduku la agano lake lilionekana. Sheria ya Mungu ilikuwa imehifadhiwa patakatifu sana kule mbinguni—sheria ambayo ilitamkwa na Mungu na kuandikwa kwa chanda chake katika mbao za mawe.TK 270.2

    Wale waliolielewa jambo hilo waliiona nguvu ya maneno haya ya Mwokozi kuliko wakati mwingine wo wote ule: “Amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka hata yote yatimie.” (Mathayo 5:18). Sheria ya Mungu ambayo ni ufunuo wa mapenzi yake na hati ya tabia yake, itadumu milele.TK 270.3

    Amri ya Sabato ipo katikati ya Amri Kumi. Roho wa Mungu aliwaonesha wanafunzi wa Neno lake kwamba walikuwa wameivunja amri hii bila kujua kwa kuipuuza siku ya Mwumbaji ya kupumzika. Walianza kuchunguza sababu za kuadhimisha siku ya kwanza ya juma. Hawakupata ushahidi wo wote kwamba amri ya nne ilikuwa imefutwa au kwamba Sabato ilikuwa imebadilishwa. Walikuwa wanatafuta kwa dhati kujua na kuyafanya mapenzi ya Mungu; sasa walionesha utii wao kwa Mungu kwa kuishika Sabato yake takatifu.TK 270.4

    Juhudi zilizokuwa zinafanyika kuiangusha imani ya waumini Waadventista zilikuwa nyingi. Wote waliona kwamba, kuupokea ukweli juu ya patakatifu pa mbinguni kulikuwa kunajumuisha matakwa na sheria ya Mungu na Sabato ya amri ya nne. Hapa ndipo kulikuwa na siri ya upinzani wa makusudi dhidi ya ufafanuzi linganifu wa Maandiko yaliyokuwa yanaonesha huduma ya Kristo katika patakatifu pa mbinguni. Watu walikuwa wanatafuta kuufunga mlango ambao Mungu alikuwa ameufungua, na kuufiingua ule ambao alikuwa ameufunga. Lakini Kristo alikuwa ameufungua mlango wa huduma ya patakatifu sana. Amri ya nne ilikuwa katika sheria iliyokuwa imehifadhiwa humo.TK 271.1

    Wale waliokuwa wameipokea nuru iliyokuwa inahusu uombezi Wakristo na sheria ya Mungu waliona kuwa huu ulikuwa ukweli wa Ufunuo 14, yaani onyo lenye sehemu tatu la kuwaandaa wakazi wa dunia kwa ajili ya Ujio wa Bwana. (Tazama kiambatisho) Tangazo lisemalo, “Saa ya hukumu yake imekuja” linatangaza ukweli ambao unapasa kuhubiriwa mpaka uombezi wa Mwokozi utakapokoma na yeye kurudi kuja kuwachukua watu wake awapeleke kwake. Hukumu ambayo ilianza mwaka 1844 itaelendelea mpaka mashauri ya watu wote, walio hai na waliokufa, yaaamuliwe; kwa hiyo itaendelea mpaka mwisho wa muda wa matazamio wa wanadamu. Ujumbe huu unawaagiza wanadamu kumcha “Mungu na kumtukuza,” na kumsujudia “yeye aliyeziumba mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.” Matokeo ya kuupokea ujumbe huu yanaelezwa: “Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu na kuwa na imani ya Yesu.” Ufunuo 14:7, 12.TK 271.2

    IIi watu wawe tayari kwa ajili ya hukumu, inawapasa kuishika sheria ya Mungu, ambayo ni kipimo cha tabia na kigezo kitakachotumika katika hukumu. Paulo anasema “Kwa kuwa wote waliokosa ... wenye sheria, watahukumiwa kwa sheria.” “Ni wale waitendao sheria watakaohesabiwa haki.” Imani ni ya lazima katika kuishika sheria ya Mungu; kwani “pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu.” “Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi.” Warumi 2:12-16; Waebrania 11:6; Warumi 14:23.TK 271.3

    Malaika wa kwanza aliwasihi watu kumcha “Mungu na kumtukuza,” na kumsujudia kama Mwumbaji wa mbingu na nchi. Inawapasa kuishika sheria ya Mungu ili waweze kufanya hivyo. bila utii, hakuna ibada inayoweza kumpendeza Mungu. “Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake.” 1 Yohana 5:3; soma Mithali 28:9.TK 272.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents