Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kuinuka Kwa Mamlaka Nyingine

    Hapa kinaanza kuelezewa kielelezo kingine: “Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo.” (Ufunuo 13:11). Taifa hili halifanani na yale yaliyotajwa kwa vielelezo vilivyotangulia. Falme kubwa zilizokuwa zimetawala dunia zilikuwa zimeoneshwa kwa nabii Danieli kama wanyama wanaoua na kula wanyama wengine, zilizoinuka wakati “pepo nne za mbinguni zilipovuma kwa nguvu juu ya bahari kubwa.” (Danieli 7:2). Katika Ufunuo 17:15 malaika mmoja alieleza kuwa maji yanawakilisha “jamaa na makutano na mataifa na lugha.” Upepo ni kielelezo cha ghasia. Pepo nne zinazovuma kwa nguvu juu ya bahari kubwa zinawakilisha matukio ya kutisha ya kuangushana na mapinduzi ambayo falme ziliyatumia kujipatia mamlaka.TK 273.4

    Lakini mnyama huyu mwenye pembe kama mwana kondoo alionekana “akipanda juu kutoka katika nchi.” Badala ya kuangusha falme zingine ili kujiimarisha, taifa hilo ni lazima litokee katika eneo ambalo halikuwa na wakazi na ilipasa likue kwa amani. Taifa hilo ni lazima litafutwe katika bara la magharibi mwa dunia.TK 274.1

    Ni taifa gani katika eneo jipya ambalo lilikuwa likiinuka kwa mamlaka mwaka 1798, likiwa na dalili za uwezo na kutambulika ulimwenguni? Ni taifa moja tu, tena moja tu, linalokidhi vigezo vya unabii huu-— Marekani. Karibu maneno yale yale ya mwandishi wa Maandiko yametumiwa bila kujua na mwanahistoria mmoja akielezea kuinuka kwa taifa hili. Mwandishi mmoja maarufu anazungumzia “fumbo la kuinuka kwake kutoka mahali patupu, ” na kusema, “Tulimea na kuwa dola kama mbegu imeayo kimya.” 227G. A. Townsend, The New World Compared With the Old, p. 462. Jarida moja la mwaka 1850 lilisema kuhusu “kuinuka” kwa Marekani na “katika ukimya wa dunia ikaongezeka katika nguvu na fahari” 228Dublin Nation.TK 274.2

    “Naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo.” Pembe kama za Mwana-Kondoo zinaonesha ujana, kutokuwa na hatia, na upole. Miongoni mwa wahamiaji wa Kikristo waliokimbilia kwanza Marekani, kutokana na ukandamizaji wa wafalme na kukosa uvumilivu kwa makasisi, kulikuwa na wengi waliokuwa wameazimia kuanzisha uhuru wa kiraia na kidini. Tamko la Uhuru [la Marekani] linaelezea ukweli kwamba, “watu wote wameumbwa sawa” na kupewa haki isiyoweza kuondolewa ya kuishi, uhuru, na kutafiita fiiraha.” Katiba [ya Marekani] inawahakikishia watu haki ya kujitawala, ikielekeza kuwa wawakilishi waliochaguliwa kwa kura za wengi watatunga na kusimamia sheria. Uhuru wa imani ya kidini pia ulitolewa. Mfumo wa jamhuri na Uprotestanti vikawa kanuni kuu za kitaifa, siri ya uwezo na mafanikio ya Marekani. Wengi wamekuwa wakitafuta kwenda huko, na Marekani imeinuka na kuwa miongoni mwa mataifa yenye nguvu kabisa duniani.TK 274.3

    Lakini lile taifa lenye pembe kama za mwanakondoo lilinena “kama joka. Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona ... akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi.” Ufunuo 13:11-14TK 275.1

    Pembe kama za mwanakondoo na sauti ya joka vinaonesha ukinzani. Utabiri kwamba atanena “kama joka” na kutumia “nguvu zote za yule mnyama wa kwanza” unaonesha roho ya kutokuvumiliana na mateso ya yule joka na yule mnyama aliye mfano wa chui. Na ule usemi kwamba yule mnyama mwenye pembe mbili “aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza,” unaonesha kwamba mamlaka ya taifa hili italazimisha utii kwa mamlaka ya Papa.TK 275.2

    Kitendo kama hicho kitakuwa kinakinzana na mfiimo wake wa taasisi huru, Tamko la Uhuru na katiba. Katiba inasema, “Bunge halitatunga sheria inayopendelea taasisi ya kidini, au kuzuia uhuru kwa kidini,” na kwamba “hakuna sharti la kidini litakalozingatiwa kama sifa ya kuchaguliwa kushika ofisi yo yote ya serikali iliyo nchini Marekani.” Katika kielelezo hiki kumeoneshwa uvunjaji wa makusudi wa mihimili hii ya uhuru. Mnyama mwenye pembe kama za mwana kondoo— ambaye kwa maneno ni msafi, mpole na asiye na madhara—atanena kama joka.TK 275.3

    “Akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama.,” Hapa imewakilishwa aina ya serikali ambapo mamlaka ya kutunga sheria yamo mikononi mwa watu, ushahidi wa wazi kwamba Marekani ndiyo taifa linalozungumziwa hapa. Lakini, sanamu ya mnyama ni nini? Itaundwa vipi.TK 275.4

    Kanisa la mwanzo lilipopotoka, lilitafuta msaada wa mamlaka za kidunia. Matokeo yake ni: mamlaka ya Papa, yaani kanisa lililokuwa linatawala serikali, na hasa katika kuwaadhibu “waasi.” Ili Marekani iunde “sanamu ya mnyama,” ni lazima mamlaka za kidini zidhibiti utawala wa kiraia kiasi kwamba serikali itatumiwa pia na kanisa kutimiza makusudi ya kanisa.TK 275.5

    Makanisa ya Kiprotestanti yaliyofuata nyayo za Kanisa la Roma yameonesha shauku kama hiyo ya kudhibiti uhuru wa dhamiri. Mfano ni mateso ya muda mrefu yaliyofanywa na Kanisa la Uingereza dhidi ya watu waliojitenga. Katika kame ya kumi na sita na ya kumi na saba, wachungaji na watu waliokuwa hawakubaliani na kanisa walitozwa faini, walifungwa, waliteswa na kuuawa.TK 276.1

    Uasi ulilifanya kanisa la awali kutafuta msaada wa serikali ya kiraia, na jambo hilo liliandaa njia kwa ajili ya mamlaka ya Papa—yaani mnyama. Paulo alisema: “Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi.” 2 Wathesalonike 2:3.TK 276.2

    Biblia inasema: “Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu; wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.” 2 Timotheo 3:1-5. “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya maShetani.” 1 Timotheo 4:1.TK 276.3

    Wote ambao “hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa,” watapokea “nguvu ya upotevu, wauamini uongo.” 2 Wathesalonike 2:10,11. Hali hii itakapofikiwa, athari zile zile zitafuata kama ilivyokuwa katika kame za mwanzo.TK 276.4

    Tofauti kubwa ya imani katika makanisa ya Kiprotestanti inachukuliwa kama ushahidi kwamba hakutakuwa na mwafaka wa lazima. Lakini kwa miaka kadhaa kumekuwa na mwelekeo miongoni mwa makanisa ya Kiprotestanti wa kutaka mwungano. Ili kuwa na mwungano wa aina hiyo, mijadala ya mambo ambayo wote walikuwa hawakubaliani itabidi iwekwe kando. Katika juhudi za kufikia mwafaka kamili, itakuwa imebaki kidogo tu kugeukia matumizi ya nguvu.TK 276.5

    Makanisa makubwa ya Marekani, yakiwa yameungana katika masuala ya mafundisho yanayoshikwa na wote, yatakapoishawishi serikali kulazimisha imani zao na kuunga mkono taasisi zao, Marekani ya Kiprotestanti itakuwa imeunda sanamu ya utawala wa Kanisa la Roma, na taabu ya adhabu za kiserikali kwa wanaopinga itafuata bila shaka.TK 277.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents