Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Onyo la Malaika wa Tatu

    Onyo la kutisha kuliko yote yaliyowahi kutolewa kwa wanadamu lipo katika ujumbe wa malaika wa tatu. Haipasi watu waachwe gizani juu ya suala hili muhimu; onyo hili halina budi kutolewa kwa ulimwengu kabla ya mapigo ya hukumu Mungu, ili wanadamu wote wawe na fursa ya kuyaepuka. Malaika wa kwanza anatangazia “kila taifa na kabila na lugha na jamaa.” (Ufunuo 14:6). Onyo la malaika wa tatu litaenea vivyo hivyo. Litatangazwa kwa sauti kuu na litavuta usikivu wa ulimwengu mzima.TK 280.2

    Watu wote watagawanyika katika makundi mawili makubwa—wale wazishikao amri za Mungu na kuwa na imani ya Yesu, na wale wanaomsujudia mnyama na sanamu yake na kupokea alama yake. Kanisa na serikali vitaungana kuwalazimisha watu “wote” kupokea “alama ya manyama,” lakini watu wa Mungu hawataipokea. Nabii Yohana aliwaona wale “wenye kushinda, watokao kwa yule mnyama, na sanamu yake, na kwa hesabu ya jina lake, walikuwa wamesimama kando-kando ya hiyo bahari ya kioo, wenye vinubi vya Mungu.” UfunuoTK 280.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents