Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sheria ya Uhuru

    Walimu wengi wa kidini wanadai kuwa kwa kifo chake, Yesu aliiondoa kabisa sheria. Baadhi wanaiwakilisha kama ni nira yenye maumivu makali na kinyume na “utumwa” wa sheria wanasisitiza “uhuru” upatikanao kwenye lnjili.TK 288.2

    Lakini sivyo manabii na mitume walivyoichukulia sheria ya Mungu. Daudi anasema, “Nami nitakwenda panapo nafasi, Kwa kuwa nimejifunza mausia yako.” Zaburi 119:45. Mtume Yakobo anarejea kwenye Amri Kumi za Mungu anaposema, “sheria kamilifu iliyo ya uhuru.” Yakobo 1:25. Mwandishi wa kitabu cha Ufunuo anatamka baraka kwa wale wazifuao nguo zao, “wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima.” Ufunuo 22:14.TK 288.3

    Kungekuwa na uwezekano wa kuibadilisha sheria au kuiweka kando, Kristo hangekufa ili kumwokoa mwanadamu kutoka kwenye adhabu ya dhambi. Mwana wa Mungu alikuja, “kuitukuza sheria, na kuiadhimisha.” Isaya 42:21. Anasema, “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati.” “Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka” Kumhusu Yeye Mwenyewe anasema, “Kuyafanya mapenzi yako, Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu; Naam, sheria yako imo moyoni mwangu.” Mathayo 5:17,18; Zaburi 40:8.TK 288.4

    Sheria ya Mungu haibadiliki, ni ufunuo wa tabia ya mtunga sheria. Mungu ni upendo na sheria ni upendo. “Pendo ndilo utimilifu wa sheria.” Mwandishi wa Zaburi anasema: “sheria yako ni kweli”; “Maana maagizo yako yote ni ya haki.” Paulo anatamka kuwa, “torati ni takatifu, na ile amri ni takatifu, na ya haki, na njema.” Warumi 13:10; Zaburi 119:142, 172; Warumi 7:12. Sheria ya namna hiyo yapaswa kuwa yenye uvumilivu kama alivyo mtunzi wake.TK 288.5

    Ni kazi ya uongofu na utakaso kuwapatanisha wanadamu na Mungu kwa kuwaleta kwenye muafaka na kanuni za sheria yake. Hapo mwanzo mwanadamu alikuwa na mapatano kamili na sheria ya Mungu. Lakini dhambi ilimtenganisha kutoka kwa Muumba wake. Moyo wake ulikuwa unapingana na sheria ya Mungu. “ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii.” Lakini, “Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee” ili mwanadamu apatanishwe na Mungu, arejeshwe kwenye mapatano na Muumba wake. Badiliko hili ni kuzaliwa upya, ambalo bila hilo “hawezi kuuona ufalme wa Mungu.” Yohana 3:16, 3.TK 289.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents