Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ni Kwa Njia ya Imani Pekee

  Kazi hii inaweza kukamilishwa tu kwa njia ya imani katika Kristo, kwa uwezo wa Roho wa Mungu aliye ndani yetu. Mkristo atahisi misukumo ya kutenda dhambi, lakini atadumisha vita visivyokoma dhidi yake. Yupo mahali ambapo msaada Wakristo unahitajika. Udhaifu wa kibinadamu unaunganishwa na uwezo wa Mungu, na imani inatamka kwa mshangao kwamba: “Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.”l Wakorintho 15:57.TK 291.1

  Kazi ya utakaso ni endelevu. Katika uongofu, mwenye dhambi anapata amani kati yake na Mungu, ndipo maisha ya Ukristo yanakuwa yameanza. Sasa anatakiwa auendee “utimilifu” kukua “hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu Wakristo” “nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mmwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.” Waebrania 6:1; Waefeso 4:13; Wafilipi 3:14.TK 291.2

  Wale wanaopitia uzoefu wa utakaso wataonesha unyenyekevu. Wanaona kutostahili kwao wakijilinganisha na ukamilifu wa Yeye asiye na ukomo. Nabii Danieli alikuwa kielelezo cha utakaso wa kweli. Badala ya kudai kwamba alikuwa safi na mtakatifu, huyo nabii aliyeheshimiwa, alijiweka kundi moja na Waebrania wenye dhambi pale alipomlilia Mungu kwa niaba ya watu wake. Danieli 9:15,18,20; 10:8, 11.TK 291.3

  Kwa wale wanaotembea katika kivuli cha msalaba wa Kalvari, hapatakuwa na kujiinua nafsi, wala kudai kwa majivuno, kwamba wapo huru dhidi ya dhambi. Wanahisi kwamba ni dhambi yao iliyosababisha maumivu makali, yaliyouvunja moyo wa Mwana wa Mungu, na wazo hili litawaongoza katika kujishusha. Wale wanaoishi karibu na Yesu, wanatambua kwa uwazi kabisa udhaifu na hali ya dhambi ya mwanadamu, tumaini lao pekee ni kafara ya Mwokozi aliYesulibiwa akafufuka.TK 291.4

  Utakaso unaopata umaarufu sasa katika ulimwengu wa kidini unabeba roho ya kujiinua nafsi na kuidharau sheria ya Mungu hata kuiona kama kitu kigeni ndani ya Biblia. Watetezi wake wanafundisha kuwa utakaso ni tukio au kazi ya mara moja, ambapo, kwa njia ya “imani pekee” wanapata utakatifu kamili. Wanasema kuwa “Amini tu” na ” na baraka itakuwa yako” Anayepokea utakaso huo haimpasi kuwa na juhudi za ziada. Sambamba na hilo wanaokataa mamlaka ya sheria ya Mungu, wakitoa hoja kwamba wako huru dhidi ya wajibu wa kutunza amri. Lakini je, inawezekana kuwa mtakatifu pasipo kufikia mapatano na kanuni zinazofunua tabia na mapenzi ya Mungu?TK 291.5

  Ushuhuda wa Neno la Mungu uko kinyume na fundisho hili lenye mtego la imani bila matendo. Si imani inayotupatia kibali mbinguni pasipo kutimiza masharti ambayo kwayo rehema itatolewa. Ni jambo la kudhaniwa tu. (soma Yakobo 2:14-24).TK 292.1

  Hebu pasiwepo watu watakaojidanganya kwamba wanaweza kuwa watakatifu wakiendelea kuvunja kwa makusudi moja ya matakwa ya Mungu. Dhambi inayofahamika hunyamazisha sauti ya Roho inayoshuhudia na huitenganisha nafsi na Mungu. Ingawa Injili na nyaraka za Yohana zimejikita kikamilifu kwenye mada ya upendo; hajasita kuifunua tabia halisi ya daraja la watu wanaodai kuwa wametakaswa huku wakiendelea kuishi maisha ya uasi dhidi ya sheria ya Mungu.TK 292.2

  “Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake. Lakini yeye alishikaye neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli.” lYohana 2:4, 5. Hapa kipo kipimo kwa kila mtu anayemkiri Yesu. Kama wanadamu watapunguza umuhimu na kuondoa uzito katika maagizo ya Mungu, ikiwa mtu ye yote atavunja, “amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo” (Mathayo 5:18, 19) tutaweza kujua kuwa madai yao hayana msingi.TK 292.3

  Madai ya kutokuwa na dhambi ni uthibitisho kuwa yeye atoaye madai hayo yu mbali na utakatifu. Hana ufahamu wa kweli juu ya usafi usio na mwisho na utakatifu wa Mungu, na ubaya na uovu wa dhambi. Kadiri anavyokuwa mbali na Yesu, ndivyo anavyozidi kujiona mwenye haki machoni pake.TK 292.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents