Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Adui Aliye Macho

    Adui huyu aliye macho anajiingiza katika kila nyumba, kila mtaa, kwenye makanisa, kwenye mabaraza ya taifa, kwenye mahakama za haki, akitatanisha, akidanganya, akishawishi, kila mahali akiharibu nafsi na miili ya wanaume, wanawake, na watoto. Anasambaratisha familia, akipanda chuki, ugomvi, uchochezi, na mauaji. Na ulimwengu unaelekea kuchukulia kwamba Mungu ameyapanga mambo hayo na hayana budi kuwepo. Wale wote ambao ni wafuasi nusu-nusu Wakristo ni watumishi wa Shetani. Wakristo wanapochagua jamii ya waovu, wanajipeleka wenyewe kwenye majaribu. Shetani anajiflcha wasimwone na kuleta vivutio vinavyodanganya machoni pao.TK 313.2

    Mapatano na desturi za kiulimwengu yanalibadilisha kanisa kuelekea kwenye ulimwengu na siyo ulimwengu kuelekea kwa Kristo. Kuzoeana na dhambi kutaifanya ionekane kuwa inatia kinyaa kidogo tu. Tunapokuwa kazini tunaletwa kwenye majaribu, tunaweza kuwa na hakika kuwa Mungu atatulinda; lakini endapo tutajiweka wenyewe chini ya majaribu tutanguka muda wowote.TK 313.3

    Mara nyingi mjaribu hufanya kazi yake kwa mafanikio makubwa kupitia wale ambao hudhaniwa kidogo sana kuwa wapo chini ya udhibiti wake. Talanta na maarifa ni vipawa vya Mungu; lakini vinapoelekezwa mbali naye, vinageuka kuwa mtego.Wengi wa watu wenye akili na maarifa na wenye mvuto ni vyombo vilivyonolewa mikononi mwa Shetani.TK 313.4

    Usisahau onyo lililovuviwa likitoa sauti tangu kame nyingi hadi wakati wetu. “Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.” “Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.” 1 Petro 5:8; Waefeso 6:11. Adui yetu mkuu anajiandaa kwa ajili ya kampeni yake ya mwisho. Wale wote wanaomfuata Yesu watakuwa katika pambano dhidi ya adui huyu. Kwa kadiri Mkristo anavyoiga kielelezo cha mbinguni, ndivyo atakavyojiweka kuwa shabaha ya mashambulizi ya Shetani.TK 314.1

    Shetani alimshambulia Yesu kwa ukali na majaribu ya werevu; lakini alishindwa katikakila pambano. Ushindi huo unatufanya sisi kushinda. Kristo atawapa uwezo wale wote wanaoutafuta. Hakuna mtu ambaye atashindwa na Shetani bila hiari yake. Mjaribu hana uwezo wa kuudhibiti utashi au kuilazimisha nafsi kutenda dhambi. Anaweza kusababisha dhiki lakini siyo unajisi. Yapasa ukweli kuwa Yesu alishinda uwavuvie wafuasi wake nguvu za kupigana vita dhidi ya dhambi na Shetani.TK 314.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents