Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Biblia Inawakilishwa Kama Riwaya

    Mitume, wakiigizwa na roho zidanganyazo, wapo kwa ajili ya kuleta ukinzani dhidi ya yale waliyoandika walipokuwepo duniani. Shetani anaufanya ulimwengu uamini kuwa Biblia ni hadithi ya kubuni; kitabu chenye manufaa tangu mwanzo wa jamii ya wanadamu, lakini sasa kinaonekana kuwa hakifai kwa matumizi. Kitabu ambacho kitamhukumu yeye na wafuasi wake anakifanya kuwa duni, Mwokozi wa ulimwengu anamfanya kuwa si zaidi ya mwanadamu wa kawaida. Na wale wanaoamini juu ya udhihirisho wa roho, wanajaribu kufanya ionekane kuwa katika maisha ya Yesu, hakuna chochote ambacho ni muujiza. Wanatangaza kuwa miujiza yao inazidi sana kazi za Kristo.TK 340.2

    Imani ya mizimu kwa sasa inachukua mtindo wa Ukristo. Lakini mafundisho yake hayawezi kukataliwa wala kufichwa. Katika sura yake ya sasa, ni udanganyifu hatari na wenye ustadi mkubwa. Imani hii inajidai sasa kumkubali Kristo na Biblia. Lakini Biblia inafasiliwa ili kuupendeza moyo ambao haujaongoka. Upendo unaelezwa sana kuwa ni tabia kuu ya Mungu, lakini umeshushwa hadhi na kuwa hisia dhaifu za moyo, na kufanya iwepo tofauti ndogo kati ya wema na uovu. Shutuma za Mungu juu ya dhambi, matakwa ya sheria yake takatifu, yamewekwa kando. Hadithi za uongo zinawaongoza watu kuikataa Biblia kama msingi wa imani yao. Kristo kwa hakika anakanwa kama alivyokataliwa mwanzo, lakini udanganyifu haujagundulika.TK 340.3

    Ni wachache wenye utambuzi halisi juu ya nguvu ya udanganyifu ya imani ya mizimu. Wengi wanashughulika nayo kwa manufaa ya udadisi tu. Wangejawa na hofu endapo wangefikiria juu ya wazo la kuwa wamepagawa na pepo. Lakini wanajihatarisha kwenye maeneo yaliyokatazwa, na mwangamizaji anaionesha uwezo wake juu yao kinyume na dhamiri zao. Hebu mara moja waelekeze akili zao upande wake, naye atawashikilia mateka. Hakuna kitakachowaokoa isipokuwa uwezo wa Mungu kwa kujibu maombi ya uaminifu.TK 340.4

    Wale wote wanaolea dhambi zinazofahamika, wanakaribisha majaribu ya Shetani. Wanajitenga wenyewe kutoka kwa Mungu na kwenye ulinzi wa malaika zake. “Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong’ona; je! Haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je! Waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai? Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi.” Isaya 8:19,20.TK 341.1

    Kama wanadamu wangehiari kupokea ukweli juu ya asili ya mwanadamu na hali ya wafu, wangeweza kuona katika imani ya mizimu uwezo wa Shetani na miujiza ya uongo. Lakini wengi wanafumba macho wasione nuru, na Shetani husokota mitego yake kuwazunguka. “Kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa.” Kwa hiyo, “Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo” 2Wathesalonike 2:10,11.TK 341.2

    Wale wanaopinga imani ya mizimu wanamchokoza Shetani na malaika zake. Shetani hataachia uwanja hata inchi moja isipokuwaTK 341.3

    kwakufukuzwa na wajumbe wa mbinguni. Anaweza kunukuu Maandiko na atapotosha mafundisho yake. Wale watakaosimama katika waakati huu wa hatari ni lazima waufahamu wenyewe ushuhuda wa Maandiko.TK 341.4

    Hizo roho za maShetani zikichukua sura za ndugu au marafiki zitavuta huruma zetu na kutenda miujiza. Ni lazima tuwashinde kwa njia ya ukweli wa Biblia kwamba wafu hawajui neno lolote na wale wanaotokea ni roho za maShetani.TK 341.5

    Wote ambao imani yao haijajengwa kwenye Neno la Mungu watadanganywa na kushindwa na Shetani. Shetani “hutenda kazi kwa udanganyifu wote wa udhalimu.” na udanganyifli yake utaongezeka. Lakini wale wanaoitafuta kweli na kuitakasa mioyo yao kwa kutii watampata ndani yake Mungu wa kweli mlinzi wa hakika. Muda si mrefu, Mwokozi atamtuma kila malaika atoke mbinguni ili kuwalinda watu wake kama asivyoiacha nafsi moja inayomtumaini kushindwa na Shetani. Wale wanaojifariji wenyewe kwa uhakika kwamba hakuna adhabu kwa mdhambi, anayeukataa ukweli ambao umewekwa na mbingu uwe ulinzi kwa ajili ya siku ya taabu, wataukubali uongo wa Shetani, udanganyifu wa kuigiza wa imani ya mizimu.TK 341.6

    Wenye dhihaka wanakejeli tamko la Maandiko juu ya mpango wa wokovu na adhabu itakayowaangukia wanaoukataa ukweli. Wanazidhuru akili zilizo finyu sana, dhaifu, na zenye mapokeo potovu kuweza kutii matakwa ya sheria ya Mungu. Wamejitoa kikamilifu kwa mjaribu, wameungana naye kwa karibu na mioyoni wamejazwa roho yake, kiasi kwamba hawana nguvu ya kujinasua kwenye mtego wake.TK 342.1

    Msingi wa kazi ya Shetani uliwekwa juu ya uthibitisho aliopewa Hawa pale Edeni: “Hamtakufa hakika.” “Siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.” Mwanzo 3:4,5. Ubunifu wa hali ya juu wa udanganyifu wake ataufikia mwisho wa wakati uliosalia. Nabii anasema “Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura,... Hizo ndizo roho za maShetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.” Ufunuo 16:13, 14.TK 342.2

    Isipokuwa wale wanaolindwa na uwezo wa Mungu kwa njia ya imani kwa Neno lake, ulimwengu wote utaingia kwenye udanganyifu wake. Watu wanakubali haraka kuliwazwa kwa usalama usio na uhakika, wataamshwa tu wakati Mungu atakapokuwa akimwaga ghadhabu yake.TK 342.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents