Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Badiliko Ndani ya Uprotestanti

    Dai limetolewa katika nchi za Kiprotestanti kwamba Ukatoliki unatofautiana kidogo sana na Uprotestanti kuliko zamani. Kumekuwa na badiliko, lakini badiliko haliko ndani ya utawala wa Papa. Ukatoliki kwa kweli unafanana sana na Uprotestanti uliopo sasa kwa sababu Uprotestanti umeharibika kwa kiasi kikubwa tangu siku za Wanamatengenezo.TK 347.3

    Makanisa ya Waprotestanti, yakitafuta kuungwa mkono na ulimwengu, yanaamini uovu wote kuwa ni wema na matokeo yake mwishoni yataamini wema wote kuwa ni uovu. Kwa sasa, kama ilivyokuwa zamani, yanaomba radhi kwa Kanisa la Roma kwa ajili ya mtazamo wao usiobadilika dhidi yake, wakiomba msamaha kwa kung’ang’ania mawazo yao kupita kiasi. Wengi wanatoa hoja kuwa giza la kiakili na kimaadili lililokuwepo zama za kati lilisaidia kuenea kwa mapokeo potovu na mateso ya Kanisa la Roma; na kwamba uwezo mkubwa wa kiakili wa wakati wa sasa na uhuru unaoongezeka katika mambo ya kidini unazuia kuinuka tena kwa hali ya kutovumiliana. Dhana kwamba hali kama hiyo ya mambo itakuwepo katika kizazi hiki chenye nuru limepuuzwa. Lakini ni lazima ikumbukwe kuwa kadiri nuru kubwa inavyotolewa, ndivyo giza linavyozidi kwa wale wanaoipotosha na kuikataa.TK 347.4

    Nyakati za giza la kiakili zilijenga mazingira mazuri kwa mafanikio ya utawala wa Papa. Nyakati za nuru kubwa ni mazingira mazuri pia. Katika vizazi vilivyopita wakati watu walipokuwa hawana ufahamu wa ukweli, maelfu walinaswa, pasipo kuona nyavu zilizokuwa zimetegwa miguuni pao. Katika kizazi hiki wengi hawauoni wavu na wanauendea kwa haraka kama vipofu. Wakati wanadamu wanapoziinua nadharia zao kupita Neno la Mungu; maarifa yanaweza kuleta madhara makubwa kuliko ujinga. Hivyo sayansi ya uongo ya siku hizi itaonesha mafanikio kwa kuandaa njia ya kuukubali utawala wa Papa, kama ulivyofanya ukosefu wa maarifa katika zama za gizaTK 348.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents