Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya 37 - Usalama Wetu Pekee

    Watu wa Mungu wanaelekezwa kwenye Maandiko Matakatifu kama usalama wao wa pekee dhidi ya mvuto wa walimu wa uongo na roho za giza. Shetani anatumia kila hila kuwazuia watu wasipate maarifa ya Biblia, ambayo ina maelezo yaliyo wazi yanayofunua udanganyifu wake. Udanganyifu mkuu wa mwisho hivi punde utawekwa wazi mbele yetu. Mpinga Kristo atafanya miujiza yake ya kushangaza mbele ya macho yetu. Udanganyifu utafanana na ukweli kwa karibu sana kiasi kwamba haitawezekana kutofautisha isipokuwa kwa kutumia Maandiko.TK 359.1

    Wale wanaojitahidi kuzishika sheria zote za Mungu, watapingwa na kubezwa. Ili kuvumilia majaribu, ni lazima wayaelewe mapenzi ya Mungu kama yalivyofunuliwa katika neno lake. Ni wale tu watakao kuwa wamezijenga akili zao kwa kweli za Biblia ndio watakaosimama katika pambano kuu la mwisho.TK 359.2

    Kabla ya kusulubishwa kwake, Mwokozi aliwaeleza wanafunzi wake kwamba angeuawa na kisha angefufuka. Lakini maneno hayo yaliondolewa akilini mwa wanafunzi. Jaribu lilipokuja, kifo cha Yesu kiliondoa kabisa matumaini yao kana kwamba alikua hajawaonya mapema. Hivyo katika unabii wakati ujeo umewekwa wazi mbele yetu kwa uwazi kama ulivyokuwa umewekwa wazi kwa wanafunzi na Kristo. Matukio yanayohusiana na kufungwa kwa mlango wa rehema na kazi ya maandalizi katika kipindi cha mateso yameelezwa wazi. Lakini watu wengi hawana uelewa wa kweli hizi muhimu, na wakati wa mateso utawakuta hawako tayari.TK 359.3

    Mungu anapotoa maonyo, anamhitaji kila mtu aliyejaliwa akili auzingatie ujumbe. Hukumu ya kutisha dhidi ya ibada ya mnyama na sanamu yake (Ufunuo 14:9-11) yapasa iwaongoze wote wajifunze maana ya alama ya mnyama na jinsi ya kuepuka kuipokea. Lakini idadi kubwa ya watu hawapendi ukweli wa Biblia, kwa sababu unapingana na tamaa za moyo wenye dhambi. Shetani anawapa udanganyifu wanaoupenda.TK 359.4

    Lakini Mungu anataka watu wadumishe Biblia na Biblia pekee, kama kipimo cha mafundisho yote na msingi wa matengenezo yote. Maoni wasomi, mambo yaliyofasiliwa kisayansi, maamuzi ya mabaraza ya kidini, sauti ya walio wengi - hakuna moja kati ya haya linaloapasa kuchukuliw kuwa ushahidi au sababu ya kupinga andiko lolote. Yatupasa kudai kwa wazi andiko linalosema “Hivi ndivyo asemavyo Bwana”. Shetani anawaelekeza watu wawaangalie wachungaji, kwa walimu wa teolojia kama miongozo yao, badala ya wao wenyewe kuyachunguza Maandiko. Kwa kuwadhibiti viongozi hawa anaweza kuwashawishi watu wengi.TK 359.5

    Kristo alipokuja, watu wa kawaida walimsikiliza kwa furaha. Lakini wakuu wa ukuhani na watu wanaoongoza,walijifungia wenyewe kwenye maono yasiyo sahihi; wakiukataa ushahidi uliodhihirisha kuwa yeye ni masihi. “Imekuwaje” watu waliuliza, “kwamba watawala wetu na waandishi wasomi hawamwamini Yesu?” Walimu kama hao waliliongoza taifa la Kiyahudi kumkataa mwokozi wao.TK 360.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents