Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Matokeo ya Kupuuzia Maombi na Kujifunza Biblia

    Kujifunza Biblia kusifanyike bila maombi. Roho mtakatifu pekee ndiye anayeweza kutufanya tuguswe na umuhimu wa mambo ambayo ni rahisi kuelewa au kutuepusha kushindana na mambo ambayo ni vigumu kuyaelewa. Malaika wa mbinguni wanauandaa moyo kulielewa Neno la Mungu. Tutavutwa na uzuri wake, tukionywa na kuimarishwa na ahadi zake. Mara nyingi majaribu yanaonekana kama yasiyopingika kwa sababu yule anayejaribiwa hawezi kuzikumbuka ahadi za Mungu na kukabiliana na Shetani kwa silaha ya Maandiko. Lakini malaika wanawazunguka wale ambao wako tayari kujifunza na wanawakumbusha ukweli unaohitajika.. . .TK 362.2

    “Yeye atakufundisha mambo yote na kukukumbusha yale yote niliyokuambia’-Yn. 14:26. Lakini sharti mafundisho ya Kristo yawe yametunzwa mawazoni ili Roho wa Mungu aweze kutukumbusha wakati wa shida.TK 362.3

    Mustakabali wa wakazi wa wanaoijaza dunia unakaribia kuamuliwa. Yampasa kila mfuasi Wakristo aombe kwa bidii: “Nifanye nini, Bwana?” Matendo 22:10.(Angalia pia Matendo 9:6.) Yatupasa tujitahidi sasa kuwa na uzoefu wa kina na ulio hai katika mambo ya Mungu. Hatuna muda wa kupoteza. Tupo katika uwanja wa Shetani. Msilale, askari wa Mungu.TK 362.4

    Wengi wanajipongeza kwa kutofanya mambo mabaya. Haitoshi wao kuwa miti katika bustani ya Mungu. Wanapaswa kuzaa matunda. Katika vitabu vya mbinguni wameandikwa kama vikwazo ardhini. Na kwa wale ambao wameichezea rehema ya Mungu na kuitumia vibaya neema yake moyo wenye upendo wa kuvumilia bado unasihi.TK 362.5

    Katika kipindi cha kiangazi kunakua hakuna tofauti iliyo wazi kati ya miti ambayo daima inakuwa na kijani kibichi na miti mingine, lakini kipindi cha upepo na baridi kinapokuja ile miti ya kijani kibichi haibadiliki wakati miti mingine inapukutisha. Hebu upinzani uje, hebu ije hali ya kutovumiliana iliyo na msukosuko, hebu mateso yachochewe tena na wale walio na mashaka na wanaflki wataiacha imani. Lakini Mkristo wa kweli atasimama imara, imani yake ikiwa imara, tumaini lake liking’aa kuliko siku za mafanikio. “Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, wala hautaacha kuzaa matunda.Yeremia 17:8.TK 363.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents