Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Mungu Analaumiwa Kwa Sababu ya Maumivu

    Lakini uchungu ambao watu wa Mungu wataupata hautakuwa hofu ya mateso. Watahofu kuwa kwa sababu ya makosa yao fulani, ahadi ya Mwokozi: “Mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi.”- Ufunuo 3:10, haitatimia kwao.. Wakidhihirisha kutostahili kwao kwa sababu ya upungufu katika tabia zao, jina takatifu la Mungu litatukanwa.TK 373.1

    Wataikumbuka toba ya zamani juu ya dhambi zao nyingi na wataomba ahadi ya mwokozi: “Au azishike nguvu zangu, Afanye amani nami; Naam, afanye amani nami.” Isaya 27:5. Hata kama watasumbuliwa na mateso, msongo na huzuni; hawataacha kuomba. Watamshika Mungu kama Yakobo alivyomshika malaika, na lugha ya roho zao itakuwa “Sitakuachia uende, mpaka unibariki.”TK 373.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents