Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kutokea kwa Mfalme wa Wafalme

    Sauti ya Bwana itasikika ikitangaza siku na saa ya kuja kwa Yesu. Israeli wa Mungu watasimama wakisikiliza, sura zao zikiangaziwa utukufu wake. Punde litaonekana upande wa mashariki wingu dogo jeusi. Ni wingu litakalomzunguka Mwokozi. Kwa ukimya mkuu watu wa Mungu watalikazia macho kadiri litakavyokaribia, hadi litakapokuwa wingu kubwa jeupe, sehemu yake ya chini kutakuwa na utukufu kama wa moto ulao, na juu yake upinde wa agano. Sasa siyo “Mtu wa huzuni,” Yesu atakuwa akija kama mshindi mkuu. Malaika watakatifu kundi kubwa lisilohesabika watakuwa pamoja naye, “kumi elfu mara kumi elfu na maelfu kwa maelfu.” Kila jicho litamwona Mfalme wa uhai. Taji ya utukufu itatulia kichwani mwake. Sura yake itang’aa kuliko jua la mchana. “Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NABWANA WA MABWANA.” Ufunuo 19:16.TK 383.4

    “Mfalme wa wafalme atashuka na wingu, lililozungushiwa moto unaowaka. Dunia itatetemeka mbele yake: “Mungu wetu atakuja wala hatanyamaza, Moto utakula mbele zake, na tufani yavuma sana ikimzunguka pande zote. Ataziita mbingu zilizo juu, Na nchi pia awahukumu watu wake.” Zaburi 50:3,4.TK 384.1

    “Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima, wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo. Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?” Ufunuo 6:15-17.TK 384.2

    Vicheko vya dhihaka vitakuwa zimekoma, midomo ya uongo itanyamazishwa. Hakuna kitakachosikika isipokuwa sauti ya maombi na sauti ya kulia. Waovu wanaomba wazikwe chini ya miamba kuliko kukutana na uso wa yule waliyemdhihaki. Sauti hiyo inayopita kwenye sikio la wafu, wanaijua. Ni mara ngapi sauti hii laini uiliwaita ili watubu? Ni mara ngapi kulisikika kusihi kwake rafiki, ndugu, Mwokozi. Sauti hiyo itaamsha kumbukumbu za maonyo yaliyopuuzwa na mialiko iliyokataliwa.TK 384.3

    Wapo wale waliomdhihaKikristo wakati wa mateso yake. Alisema: “Tangu sasa mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu ya mbinguni.” Mathayo 26:64. Sasa watamwona katika utukufu wake; na tena watamwona akiwa ameketi katika mkono wa kuume wa mamlaka. Pale atakuwepo Herode mwenye kiburi aliyezomea akiwa na cheo chake cha ufalme. Watakuwepo hapa watu ambao walimvisha kichwani taji ya miiba na mkononi mwake wakampa fimbo ya kifalme - wale waliosujudu mbele yake kwa dhihaka ya kukufuru, wale waliomtemea mate mfalme wa uzima. Watataka kukimbia mbele zake. Wale walioipigilia misumari kwenye mikono na miguu yake wataziangalia alama kwa hofu na majuto.TK 384.4

    Kwa uwazi wa kutisha makuhani na watawala watakumbuka matukio ya Kalvari, jinsi walivyokuwa wakitikisa vichwa katika mizaha ya kishetani, wakapaza sauti na kusema, “Aliokoa wengine; hawezi kujiokoa mwenyewe.” Mathayo 27:42. Huku wakipaza sauti kwa nguvu kuliko ile waliyoitoa ikasikika Yerusalemu yote wakisema, “asulibiwe, asulibiwe! Sasa watatoa kilio cha kukata tamaa, “Ni Mwana wa Mungu!” Watatafuta kukimbia kutoka mbele ya Mfalme wa wafalme.TK 385.1

    Katika maisha ya wale wote wanaoukataa ukweli kuna wakati ambapo dhamiri huamka, wakati ambapo nafsi inasumbuka kwa majuto ya bure. Lakini haya ni kidogo kuliko majuto ya siku ile? Katikati ya hofu yao kuu watasikia sauti za watakatifu zikisema: “Tazama, huyu ndiye Mungu wetu, Ndiye tuliyemngoja atusaidie.” Isaya 25:9.TK 385.2

    Sauti ya Mwana wa Mungu itawaita watakatifu waliolala. Duniani kote wafu wataisikia sauti hiyo, na wale watakaoisikia wataishi, jeshi kubwa kutoka kila taifa, kabila, lugha na jamaa. Watatoka katika nyumba ya gereza la kifo, wakiwa wamevikwa utukufu wa kutokufa., wakilia: “Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako?” 1 Wakorintho 15:55.TK 385.3

    Wote watatoka makaburini wakiwa na kimo kilekile walichokuwa nacho wakati wanazikwa makaburini. Lakini wote watainuka wakiwa na upya wa uzima na nguvu za ujana wa milele Kristo alikuja kurejesha kile kilichopotea. Ataibadilisha miili yetu yenye dhambi na kuiumba iwe kama mwili wake wa utukufu. Miili yetu ya kufa na kuharibika ambayo hapo awali ilichafuliwa na dhambi, itakuwa haina dosari, mizuri na isiyopatwa na mauti. Dosari na ulemavu vitaachwa kaburini. Waliokombolewa “Watakua” (Malaki 4:2) kufikia kimo kamili cha mwanadamu akiwa katika utukufu wake wa mwanzo, dalili za mwisho za laana ya dhambi zitakuwa zimeondolewa. Waaminifu Wakristo katika akili na roho na mwili wataakisi sura ya Bwana wao.TK 385.4

    Wenye haki walio hai watakuwa wamebadilishwa “Kwa dakika moja, kufumba na kufumbua.” Kwa sauti ya Mungu watabadilishwa kuwa na hali ya kutokufa pamoja na watakatifu waliofufuliwa watachukuliwa ili kukutatana na Mwokozi wao angani. Malaika “watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.” Mathayo 24:31. Watoto wadogo watabebwa na kukabidhiwa kwa mikono ya mama zao. Marafiki ambao kwa muda mrefu walikuwa wametenganishwa na kifo sasa wataungana tena, kamwe hawatatengana, na kwa nyimbo za furaha watapaa pamoja kwenda katika mji waTK 386.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents