Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya 41 - Dunia Ikiwa Magofu

    Wakati sauti ya Mungu itakapowarudisha watu wake waliotekwa, kutakuwa na utambuzi wa kuogofya kwa wale waliopoteza yote katika pambano kuu la maisha. Wakiwa wamepotoshwa na udanganyifu wa Shetani, matajiri walijisifia wenyewe juu ya ubora waliokuwa nao dhidi ya wasiokuwa na kitu. Walipuuzia kuwapa chakula wenye njaa, kuwavisha waliokuwa uchi, kutenda haki, na kupenda rehema. Sasa watakuwa wamenyang’anywa vyote vilivyowafanya kuwa wakuu na kuachwa katika umaskini. Kwa hofu watashuhudia kuangamizwa kwa sanamu zao. Waliuza roho zao kwa anasa za dunia na hawakujitajirisha kwa Mungu. Maisha yao yameshindwa, anasa zao zimegeuka kuwa uchungu. Mafanikio ya maisha yote yamefagiliwa mbali kwa muda mfupi. Matajiri wataombelezea uharibifu wa majumba yao, na kutawanywa kwa dhahabu na fedha zao, na hofu kwamba wao pia wataangamia pamoja na sanamu zao. Waovu wataomboleza kwamba hayo ndiyo matokeo, lakini hawatatubu kwa ajili ya uovu wao.TK 391.1

    Mchungaji aliyeutoa kafara ukweli ili apate kupendwa na watu sasa atautambua ushawishi wa mafundisho yake. Kila mstari ulioandikwa, kila neno lilitamkwa lililowafanya watu kubaki kwenye udanganyifu lilikuwa likitawanya mbegu; na sasa atayaona mavuno. Asema Bwana: “Ole wao wachungaji, wanaoharibu kondoo za malisho yangu na kuwatawanya!...Tazama, nitawapatiliza uovu wa matendo yenu.” “Kwa kuwa ninyi mmemhuzunisha moyo mwenye haki kwa uongo, ambaye mimi sikumhuzunisha; na kuitia nguvu mikono ya mtu mbaya, hata asigeuke, na kuiacha njia yake mbaya, na kuhifadhika.” Yeremia 23:1,2; Ezekieli 13:22.TK 391.2

    Wachungaji na watu wataona kuwa wameasi dhidi ya Mwanzilishi wa sheria zote za haki. Kuweka kando sheria za Mungu kulitoa fursa ya kuibuka kwa vyanzo vingi vya uovu, hadi dunia ikawa shimo moja kubwa la uovu. Hakuna lugha itakayoweza kueleza shauku watakayoihisi wasiowaaminifu kwa ajili ya kile walichokipoteza milele-Uzima wa milele.TK 391.3

    Watu watalaumiana wao kwa wao kwa kuongozwa katika uharibifu, lakini wote wataungana katika kurundika shutuma zao chungu kwa wachungaji wasiokuwa waaminifu waliotabiri “maneno laini,” (Isaya 30:10), waliwaongoza wasikilizaji wao kuifanya tupu sheria ya Mungu na kuwatesa wale walioishika. “Tumepotea” watalia, “na ninyi ndio sababu” Mikono ambayo wakati fulani iliwavika taji heshima itainuka ili kuwaangamiza.. Kila mahali kutakuwa fujo na umwagaji wa damu.TK 392.1

    Mwana wa Mungu na wajumbe wa mbinguni wamekuwa katika mapambano dhidi ya yule mwovu ili kuwaonya, kuwaangazia, na kuwaokoa watoto wa wanadamu. Sasa wote wamefanya uamuzi; waovu wameungana kikamilifu na Shetani katika vita yake dhidi ya Mungu. Pambano halipo kwa Shetani peke yake bali pia kwa wanadamu “Maana Bwana ana mashindano na mataifa.” Yeremia 25:31.TK 392.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents