Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Shambulizi la Mwisho Dhidi ya Mungu

    Shetani atashauriana na watu hawa wenye nguvu. Watasema kwamba jeshi lililo ndani ya mji ni dogo likilinganishwa na la kwao na kwamba wataweza kulishinda. Mafundi wenye ujuzi watatengeneza zana za vita. Viongozi wa kijeshi watawapanga watu wapenda vita katika makundi na vikosi.TK 397.2

    Hatimaye amri ya kusonga mbele itatolewa, na jeshi lisilohesabika litasonga mbele, jeshi hili litakuwa kubwa kiasi kwamba muungano wa majeshi ya zama zote hautalingana nalo. Shetani, ataongoza kikosi cha mstari wa mbele, Wafalme na mashujaa wake watakuwa kwenye msururu wake. Kwa umakini wa kijeshi wanajeshi wakiwa wamejipanga kwenye mistari kulingana na vyeo vyao, watasonga mbele juu ya uso wa nchi uliobomolewa, wakiuelekea mji wa Mungu.. Kwa amri ya Yesu, malango ya Yerusalemu Mpya yatafungwa, na majeshi ya Shetani yatajipanga tayari kwa mapambano.TK 397.3

    Sasa Kristo ataonekana mbele za adui zake. Mbali juu ya mji, juu ya msingi wa dhahabu itakayokuwa iking’aa kutakuwa na kiti cha enzi. Juu ya kiti hiki cha enzi atakaa Mwana wa Mungu, na kumzunguka kutakuwa na watu wa ufalme wake. Utukufu wa Baba wa milele utamfunika Mwana wake. Mng’ao wa uwepo wake utavuka malango, na kuifunika dunia kwa nuru yake.TK 397.4

    Karibu na kiti cha cnzi watakuwapo wale ambao hapo zamani walikuwa na bidii katika kazi za Shetani, lakini wakatolewa kama vinga vya moto, wakamfuata Mwokozi wao kwa kujitoa kikamilifu. Baada yao ni wale waliokuwa wakamilifu katika tabia zao katikati ya uwongo na ukafiri, walioiheshimu sheria ya Mungu ulimwengu ulipotangaza kuwa rasmi kuwa haikuwa halali, na mamilioni, wa zama zote waliouawa kwa sababu ya imani yao. Baada ya hao ni “mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, . . . wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao.” Ufunuo 7:9. Vita vyao vitakuwa vimekoma, ushindi wao watakuwa wameupata. Tawi la mtende ni ishara ya ushindi, mavazi meupe yanawakilisha haki ya Kristo ambayo sasa ni yaoTK 398.1

    Katika mkutano huo mkubwa hakuna hata mmoja atakayedai kuwa amejipatia wokovu kwa wema wake mwenyewe. Hakuna kitakachosemwa kuhusu mateso waliyoyapitia; ujumbe wa kila wimbo mkuu ni, Wokovu ni kwa Mungu wetu na kwa Mwana- Kondoo wake.TK 398.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents