Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Hukumu Yatolewa Dhidi Ya Waasi

  Kutawazwa kwa Kristo kutafanyika mbele ya mkutano wa wakazi wa duniani na wa mbinguni. Na sasa akiwa amevikwa enzi na nguvu, Mfalme wa wafalme atatoa hukumu kwa waasi ambao waliasi sheria na kuwatesa watu wake. “Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.” Ufunuo 20:11,12.TK 398.3

  Macho ya Yesu yatakapowaangalia waovu, wataitambua kila dhambi ambayo waliwahi kuitenda. Wataona ni wapi miguu yao ilitanga pembeni mbali na njia ya utakatifu. Majaribu yenye kushawishi ambayo waliyawezesha kwa kuendekeza dhambi, wajumbe wa Mungu waliopuuzwa, maonyo yaliyokataliwa, mawimbi ya rehema yaliyorudishwa nyuma kwa ukaidi, moyo usiotubu-yote yataonekana kana kwamba yaliandikwa kwa herufi za moto.TK 398.4

  Juu ya kiti cha enzi, msalaba utafunuliwa. Kama kulivyo kuonekana kwa sinema, yataonekana mazingira ya anguko la Adamu na hatua zilizofuata za mpango wa ukombozi. Kuzaliwa kwa unyenyekevu kwa Mwokozi; maisha yake ya kawaida; ubatizo wake Yordani; kufunga na kujaribiwa jangwani; huduma yake akiwafunulia watu baraka za mbinguni; siku zilizojazwa na matendo mengi ya rehema, siku ambazo alitumia usiku mzima akiomba milimani, mitego ya husuda na roho ya chuki ambayo iligeuka kuwa faida kwake; uchungu usioelezeka katika bustani ya Gethsemane akibeba uzito wa dhambi za ulimwengu; usaliti uliomtia mikononi mwa kundi la wauaji; matukio katika usiku ule wa kutisha - mfungwa asiye na upinzani aliyeachwa na wanafunzi wake, akiwa mtuhumiwa mbele ya behewa la kuhani mkuu, ndani ya ukumbi wa hukumu wa Pilato, mbele ya Herode mwoga, kufanyiwa mzaha, kutukanwa, kuteswa na kuhukumiwa kifo -yote yataoneshwa wazi.TK 399.1

  Na sasa mbele ya makutano wanaosukwasukwa yatafunuliwa matukio ya mwisho: mteswaji mwenye subira akipita njia ya kwenda Kalvari; Mfalme wa mbinguni akining’inia msalabani; makuhani na walimu wa sheria wakidhihaki mateso yake; giza lisilokuwa la kawaida ambalo lililionesha alama ya wakati ambapo mkombozi wa ulimwengu alitoa uhai wake.TK 399.2

  Mambo ya kutisha yataonekana jinsi yalivyo. Shetani na wafuasi wake hawatakuwa nguvu ya kuacha kuiangalia picha nzima. Kila mhusika ataikumbuka sehemu yake aliyohusika. Herode aliyewachinja watoto wasiokuwa na hatia wa Bethlehemu; Herodia mwovu, ambaye damu ya Yohana Mbatizaji inadaiwa katika nafsi yake; Pilato, mtu dhaifu, aliyetumika kujaza wakati tu; askari wenye kudhihaki; halaiki ya watu iliyokuwa na hasira iliyopiga kelele, “damu yake iwe juu yetu, na juu ya watoto wetu!” -wote watatafuta kujificha mbali na uso wa mwenye enzi wa mbinguni bila mafanikio, wakati waliokombolewa wakitupa taji zao miguuni pa Mwokozi, wakisema, “alikufa kwa ajili yangu!”TK 399.3

  Atakuwapo Nero, jitu la kutisha kwa ukatili na tabia mbaya, akitazama kutukuzwa kwa wale ambao aliwahi kuwatesa, na ambao katika kuteseka kwao yeye alipata furaha yake ya kishetani. Mama yake ataishuhudia kazi yake, jinsi tamaa iliyohamasishwa na mvuto namfano wake ilivyozaa matunda ya uhalifu ulioufanya ulimwengu utetemeke.TK 399.4

  Watakuwape makasisi wa Kikatoliki na wasaidizi wao waliodai kuwa ni mabalozi Wakristo, lakini bado walitumia magereza ya chini ya ardhi, vitanda vya kutesea na kuchoma watu kwenye nguzo za moto ili kuwatawala watu wake. Watakuwapo pia wale maaskofu wenye kiburi waliojitukuza juu ya Mungu na wakajichukulia madaraka ya kuibadili sheria ya Mungu aliye juu. Makasisi hawa waliojidai watakuwa na kesi ya kujibu mbele za Mungu. Wakiwa wamechelewa sana ndipo wataona kuwa Yeye mwenye kujua yote anao wivu kwa sheria yake. Sasa ndipo watajifunza kwamba Kristo anatambua mambo mazuri yaliyo kwa watu wake wanaoteseka.TK 400.1

  Ulimwengu wote wa waovu utasimama ukishitakiwa kwa makosa ya uhaini wa hali ya juu dhidi ya serikali ya mbinguni. Hawatakuwa na yeyote wa kumsihi awasaidie; hawatakuwa na udhuru; na hukumu ya kifo cha milele itatolewa dhidi yao.TK 400.2

  Waovu wataona kile walichopoteza kwa sababu ya uasi wao. “yote haya” roho zilizopotea zitalia, ” ningekuwa nayo. Ah nimepumbazwa ajabu! Nimebadilisha amani, furaha, na heshima kwa kuchukua huzuni, aibu na kukata tamaa.” Wote wataona kuwa kutengwa kwao na mbingu ni haki. Kwa maisha yao walitamka, “Mtu huyu Yesu hatatutawala.”TK 400.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents