Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Jerome Ajisalimisha kvva Baraza

    Kukiukwa kwa hati ya usalama ya Huss kulikuwa kumeibua dhomba ya ghadhabu. Baraza lilikusudia, badala ya kumchoma Jerome, limlazimishe afute kauli zake. Alipewa nafasi ya kuchagua kati ya kukana mafundisho yake au kufa kwa kuchomwa moto. Huku akiwa amedhoofishwa na ugonjwa, taabu za gerezani na mateso na fadhaa na mashaka, kutenganishwa na marafiki na kuumizwa na kifo cha Huss, ustahimilivu wa Jerome ulikwisha. Alikiri mwenyewe kufuata imani ya Kanisa la Roma na akakubali kauli ya baraza ya kumshutumu Wycliffe na Huss, isipokuwa, “ukweli mtakatifu” 27Ibid., ch. 19 walioufundisha.TK 71.3

    Lakini katika upweke gerezani mwake aliona dhahiri kile alichokuwa amekifanya. Alifikiri juu ya ujasiri na uaminifu wa Huss kisha akatafakari juu ya jinsi yeye mwenyewe alivyokana ukweli. Alifikiri juu ya Bwana wa mbinguni ambaye kwa ajili yake alivumilia msalaba. Kabla hajarudi nyuma alikuwa amepata amani kati ya mateso katika uhakika wa upendeleo wa Mungu, lakini sasa, majuto na wasiwasi vilitesa roho yake. Alijua kuwa alitakiwa kufuta kauli nyingine kabla ya kupatana kikamilifu na Roma. Njia aliyokuwa akiingia ingeishia tu katika uasi kamili.TK 72.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents