Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Ukweli Kwenye Ngazi ya Pilato

    Ahadi ya kibali cha msamaha wa dhambi ilikuwa imetolewa na Papa kwa wote ambao wangepanda kwa magoti yao “Ngazi ya Pilato” ambayo inasemekana kuwa ililetwa kwa muujiza kutoka Yerusalemu hadi Roma. Siku moja Luther alikuwa akipanda ngazi hizi wakati sauti kama ya radi iliposikika kana kwamba inasema: “Mwenye haki ataishi kwa imani.” Warumi 1:17. Alisimama ghafla kwa miguu yake kwa aibu na hofii. Tangu wakati huo aliuona kwa usahihi zaidi uongo juu ya kuzitumainia kazi za mwanadamu kuupata wokovu. Aliugeuza uso wake kutoka Roma. Tangu wakati huo utengano uliendelea kukua hadi pale alipovunja uhusiano wote aliokuwa nao na kanisa la Papa.TK 81.2

    Baada ya kurejea kutoka Roma, Luther alipata shahada ya uzamivu katika teolojia. Sasa alikuwa huru kujikita kwenye Maandiko aliyokuwa anayapenda. Aliapa kwa dhati kuwa angelihubiri Neno la Mungu kwa ujasiri, na siyo mafu”ndisho ya Mapapa. Hakuwa tu mtawa wa kawaida, bali mjumbe wa Biblia mwenye mamlaka aliyeitwa kama mchungaji kulilisha kundi la Mungu lililokuwa na njaa na kiu ya ukweli. Alitamka kwa ujasiri kwamba Wakristo hawakupaswa kuyapokea mafundisho mengine zaidi ya yale yatokayo kwenye mamlaka ya Maandiko Matakatifu.TK 81.3

    Makundi ya watu wenye shauku waliyaelewa maneno yake. Habari za furaha juu ya upendo wa Mwokozi, uhakika wa msamaha na amani kupitia damu yake ya upatanisho zilileta furaha mioyoni mwao. Pale Wittenberg taa iliwashwa ambayo mionzi ya nuru yake ingeendelea kuongeza mng’ao wake hadi mwisho wa wakati.TK 82.1

    Lakini kuna ukinzani kati ya ukweli na uongo. Mwokozi wetu alitamka mwenyewe kuwa: “Sikuja kuleta amani, bali upanga.” Mathayo 10:34. Miaka michache baada ya kuanza kwa Matengenezo, Luther alisema: “Mungu...ananisukuma kwenda mbele...ninatamani kuishi kwa utulivu; lakini nimetupwa katikati ya misukosuko na mapinduzi” 41Ibid., bk. 5, ch. 2.TK 82.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents