Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya 1 - Utabiri Wa Hatima Ya Dunia

    Yesu aliutazama mji wa Yerusalemu kutoka katika kilele cha mlima wa mizeituni. Majengo mazuri ya hekalu yalikuwa yanaonekana vizuri. Jua lililokuwa linatua liliuangazia weupe wa kuta zake za marumaru zake uliokuwa kama theluji na kuufanya ule mnara wa dhahabu ung’ae. Hakuna mwana wa Israeli ambaye angeweza kuitazama mandhari hii bila kusisimka kwa furaha na mshangao! Lakini moyo wa Yesu ulikuwa unawaza mambo mengine. “Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia.” Lk. 19:41.TK 20.1

    Yesu alikuwa halii kwa ajli yake, ingawa mbele yake kulikuwa na Gethsemane, mahali pa uchungu mkali ambapo hapakuwa mbali sana, na Kalvari, mahali ambapo angesulubiwa. Lakini matukio hayo siyo yaliyokuwa yanaleta huzuni kwake katika saa hii ya furaha. Alikuwa anawalilia maelfu ya watu wa Yerusalemu ambao wangeangamia.TK 20.2

    Historia ya zaidi ya miaka elfu moja ya fadhila maalum za Mungu kwa wateule wake ilionekana machoni mwa Yesu. Yerusalemu ilikuwa imeheshimiwa na Mungu kuliko ulimwengu wote. Bwana alikuwa “ameichagua Sayuni ... akae ndani yake.” Zab. 132:13. Manabii watakatifu walikuwa wametoa ujumbe wa onyo kwa muda mrefu. Damu ya wana kondoo ilikuwa ikitolewa kila siku, ikimwakilisha Mwana kondoo wa Mungu.TK 20.3

    Kama Israeli, kama taifa, wangedumisha utii wao kwa Mbingu, Yerusalemu ingesimama milele kama mji mteule wa Mungu. Lakini historia ya wale watu waliofadhiliwa ilikuwa ni hadithi ya kurudi nyuma na uasi. Kwa upendo wenye huruma ulio mkubwa kuliko wa baba, Mungu “aliwahurumia watu wake, na makao yake.” 2 Nya. 36:15. Kusihi na kukemea kuliposhindwa, alituma zawadi bora kuliko zote kutoka mbinguni, yaani, Mwana wa Mungu mwenyewe, ili ausihi mji huu usiokuwa na toba.TK 20.4

    Bwana wa nuru na utukufu alikuwa ameingia na kutoka kati ya watu wake kwa miaka mitatu, “akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi, ” akiwaweka huru wale waliokuwa wamefungwa, akiwapa kuona waliokuwa vipofu, akiwainua walemavu na kuwawezesha kutembea na kuwapa viziwi kusikia, akitakasa wenye ukoma, akifufua waliokufa, na akihubiri Injili kwa maskini. Soma Mdo. 10:38; Lk. 4:18; Mt. 11:5.TK 20.5

    Kama msafiri asiye na makazi, aliishi kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya watu na kupunguza tabu zao, akiwasihi waipokee karama ya uzima. Mawimbi ya rehema, yaliyosukumiwa mbali na watu hao waliokuwa na mioyo migumu, yalirudi tena kama wimbi kubwa zaidi la upendo usioelezeka uliojaa huruma. Lakini Israeli ilikuwa imemwacha Rafiki yake mkubwa na Msaada wake wa pekee. Kusihi kwa upendo wake kulipuuzwa.TK 21.1

    Saa ya tumaini na msamaha ilikuwa inapita upesi. Wingu ambalo lilikuwa likikusanyika kwa kame nyingi za uasi lilikuwa limekaribia kuinyeshea jamii hii yenye hatia. Yeye ambaye peke yake angeokoa watu kutoka katika hatima iliyokuwa imekaribia sana alikuwa amepuuzwa, ametukanwa, amekataliwa, na alikuwa anakaribia kusulubiwa.TK 21.2

    Kristo alipoutazama Yerusalemu, maangamizi ya mji mzima, taifa zima, yalionekana mbele yake. Alimwona malaika anayeangamiza akiwa na upanga ulioinuliwa kuelekea kwenye mji huo ambao kwa muda mrefu ulikuwa makazi ya Mungu. Kutoka mahali ambapo baadaye Tito na jeshi lake walisimama, alitazama hadi ng’ambo ya bonde kwenye nyua takatifu na varanda zenye matao. Kwa macho yaliyojaa machozi aliziona kuta zikiwa zimezingirwa na majeshi ya kigeni. Alivisikia vishindo vya wanajeshi wakijipanga kwa ajili ya vita, na sauti za akina mama na watoto wakililia mkate katika mji uliokuwa umezingirwa. Aliiona nyumba takatifu ya mji huo, ikulu zake na vinara vyake, vyote vikiteketeaa kwa moto, naam, rundo la vifusi vinavyofuka moshi.TK 21.3

    Alipoitazama miaka ya baadaye, aliona watu wa agano wakiwa wametawanyika katika kila nchi, “kama vipande vya chombo kilichosambazwa na dhoruba katika jangwa.” Huruma ya Mungu, upendo wa kina, vilisikika katika maneno ya huzuni: “Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hamkutaka!” Mt. 23:37.TK 21.4

    Alipoitazama Yerusalemu, Kristo aliona kielelezo cha ulimwengu uliokubuhu kwa kutokuamini na uasi, ukielelekea upesi kwenye hukumu za haki za Mungu. Moyo wake uliguswa na huruma kwa ajili ya watu wanaopata taabu na kuteseka duniani. Alitamani kuwapumzisha wote. Alikuwa radhi kuitoa nafsi yake hadi kufa ili auelete wokovu mahali wanapoweza kuufikia.TK 22.1

    Mfalme wa mbinguni akilia! Tukio hilo linaonesha ugumu wa kazi ya kuwaokoa waovu kutoka katika athari za kuvunja sheria ya Mungu. Yesu aliona kwamba ulimwengu ulikuwa katika udanganyifu kama ule uliosababisha maangamizi ya Yerusalemu. Dhambi kubwa ya Wayahudi ilikuwa kumkataa Kristo; dhambi kuu ya ulimwengu itakuwa kuikataa sheria ya Mungu, ambayo ni msingi wa serikali yake ya mbinguni na duniani. Mamilioni ya watu walio katika utumwa wa dhambi, wanaokabiliwa na mauti ya pili, watakataa kusikiliza maneno ya kweli katika siku ya kujiliwa kwao.TK 22.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents