Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Masumbuko Makali Moyoni Sasa Vamshinikiza Luther

    Wafuasi wakuu wa utawala wa Papa walidai kwamba uhalifu huo ulikuwa ni matunda ya mafundisho ya Luther. Shitaka hili lingemsababishia Mwanamatengenezo huzuni kuu ili kusudi la ukweli lifedheheshwa kwa kuwekwa kundi moja na uovu wa wenye itikadi kali. Kwa upande mwingine viongozi wa uasi walimchukia Luther. Si tu kwamba alikanusha madai yao ya kuvuviwa na Mungu lakini alisema kuwa walikuwa wameasi mamlaka ya serikali. Nao walimjibu kwa kisasi wakimshtumu kama mdanganyifu mkubwa.TK 124.2

    Wafuasi wa Kanisa la Roma walitegemea kuporomoka kwa Matengenezo. Walimlaumu Luther hata kwa makosa aliyokuwa anajaribu kwa bidii kuyasahihisha. Upande wa wenye itikadi kali, walidai kwa udanganyifu kuwa hawakutendewa haki, walipata watu wa kuwaonea huruma na wakachukuliwa kama wafia dini. Hivyo ndivyo walivyotendewa wale waliokuwa wanapinga Matengenezo, walihurumiwa na kupongezwa. Hii ilikuwa ni kazi ya roho ileile ya uasi ambayo ilidhihirishwa kwanza kule mbinguni.TK 124.3

    Bila kukoma, Shetani anatafuta kuwadanganya wanadamu na kuwaongoza kuiita dhambi kuwa ni haki na haki kuiita dhambi. Utakatifu wa kughushi, utakaso wa uongo, bado vinaendelea kuonesha hadharani roho ileile kama ilivyokuwa siku za Luther, vikiivuta mioyo ya watu kutoka kwenye Maandiko Matakatifu na kuwaongoza wanadamu kufuata hisia na maono kuliko sheria ya Mungu.TK 125.1

    Bila kuogopa, Luther aliilinda Injili kutokana na mashambulizi. Kwa kutumia Neno la Mungu alipambana na mamlaka iliyokuwa imetwaliwa na Papa, na wakati huo akisimama thabiti kama jabali dhidi ya wenye itikadi kali waliotaka kuungana na Wanamatengenezo.TK 125.2

    Kila kimoja cha vikundi hivi vya upinzani kiliyaweka kando Maandiko Matakatifu, huku vikitukuza hekima ya kibinadamu kama chanzo cha ukweli. Imani katika mantiki huifanya akili kuwa sanamu na kulifanya hili kuwa kigezo cha dini. Dai la Kanisa la Roma kwamba wana uvuvio unaoanzia kwa mitume, huwapa fursa za kufanya ubadhirifu na ufisadi ulioflchwa chini ya vazi la agizo la kitume. Uvuvio uliodaiwa kumshukia Munzer ulianza kutoka katika fikra na mawazo yasiyo na maana. Ukristo wa kweli hulipokea Neno la Mungu kama kipimo kuthibitisha uvuvio wa aina zote.TK 125.3

    Aliporudi kutoka Wartburg, Luther alimalizia kutafsiri Agano Jipya, na baada ya muda mfupi baadaye, Injili ilitolewa kwa Wajerumani kwa lugha yao. Toleo hili liliwafurahisha sana waliokuwa wanapenda ukweli.TK 125.4

    Makasisi waliingiwa na hofu walipotambua ya kwamba watu wa kawaida wangekuwa na uwezo wa kujadiliana nao Neno la Mungu na hivyo ujinga wao ungewekwa wazi. Kanisa la Roma lilitoa agizo kwa mamlaka yake kuzuia usambazaji wa Maandiko. Lakini kwa kadri Kanisa la Roma lilivyojaribu kupiga marufuku Biblia, ndivyo lilivyozidisha shauku ya watu kutaka kuelewa mafundisho yake. Wale walioweza kusoma walitembea nayo wala hawakuridhika mpaka hapo walipokuwa wamekariri sehemu kubwa ya Maandiko. Mara moja Luther alianza kutafsiri Agano la Kale.TK 125.5

    Maandiko ya Luther yalipokelewa kwa namna moja mijini na katika vitongoji. “Kile walichokuwa wameandika Luther na wenzake, wengine walikisambaza. Baada ya kujithibitishia wenyewe uharamu wa wajibu waliokuwa wamepewa, ingawaje walikuwa hawalijui Neno la Mungu, ...watawa walikuwa wanaviuza vitabu vya Luther na wenzake. Kwa muda mfupi Ujerumani ikajaa Walnjilisti wa vitabu waliokuwa jasiri.” 115Ibid. bk. 9, ch. 11.TK 126.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents