Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Ngurumo ya Apizo la Kanisa

    Apizo la utawala wa Papa lilinguruma dhidi ya Geneva. Ni kwa namna gani mji huu mdogo ungeweza kustahimili utawala huu msonge wenye nguvu uliokuwa umewalazimisha wafalme na wafalme wakuu kusalimu amri?TK 150.2

    Ushindi wa kwanza wa Wanamatengenezo ulikuwa umepita, Roma iliyakusanya majeshi yake upya ili kufanya maangamizi. Chama cha watu katili mno, na waliokuwa na tabia mbaya sana cha Majesuti kilianzishwa, chama hiki kilikuwa na nguvu kuliko vyama vingine vyote vilivyokuwa vinatetea utawala wa Papa. Wakiwa hawana chembe yoyote ya huruma, na dhamiri zao zikiwa zimetiwa ganzi kabisa, hawakuwa wanajua kanuni yoyote, wala uhusiano na mtu yeyote isipokuwa ule wa chama chao. (Angalia Kiambatisho)TK 150.3

    Injili ya Kristo ilikuwa imewawezesha wafuasi wake kuvumilia mateso, ama kutotishwa na baridi, njaa, kazi za sulubu, na ufukara, kutetea ukweli mbele ya mateso makali, kuwekwa kwenye magereza chini ya ardhi, au nguzo ya kuchomea watu moto. Ujesuti ulikuwa umewafundisha wafuasi wake kufanya mambo pasipo kutumia akili na kuwawezesha wao pia kuvumilia hatari kama hizo na kuipinga nguvu ya ukweli kwa silaha zote za udanganyifu. Hakuna uhalifu wowote mkubwa walioshindwa kuutenda, ama udanganyifu mbaya sana kuufanya, au kushindwa kujibadilisha sura ili kutimiza kusudi lao. Walikuwa wamejifunza hivyo kwa nia ya kuuangusha Uprotestanti na kuanzisha upya ubora wa utawala wa Papa.TK 150.4

    Walijivika mavazi ya utakatifu, walikuwa wanatembelea magereza na mahospitali, wakiwahudumia wagonjwa na maskini, huku wakilichukua jina takatifu la Yesu, walikwenda huku na huko wakitenda mema. Lakini chini ya mwonekano huu wa nje usio na hatia walikuwa wameficha uhalifu na makusudi ya kutisha.TK 151.1

    Ilikuwa ni kanuni ya msingi ya chama hiki kwamba matokeo ya mwisho wa jambo ndiyo yaliyohalalisha njia iliyotumika. Udanganyifu, wizi, kusema uongo baada ya kiapo cha kusema ukweli, mauaji ya watu maarufu, vilikuwa vinapongezwa kama vilikuwa vimefanywa kwa manufaa ya kanisa. Kwa kujigeuza umbo ili kudanganya, Majesuti walijipenyeza kwenye maofisi ya serikali, wakipanda vyeo mpaka kuwa washauri wa wafalme na kuzitengeneza walivyotaka sera za mataifa. Walikuwa watumishi ili kuwapeleleza wakuu wao. Walianzisha vyuo kwa ajili ya wakuu na waungwana, na pia walianzisha shule kwa ajili ya watu wa kawaida. Watoto wa Waprotestanti walivutwa kutunza kanuni za kidini za Kanisa la Papa. Kwa hiyo ule uhuru wa mtu kufanya anavyotaka uliopatikana kwa taabu na kumwaga damu ulisalitiwa na watoto wao. Popote Majesuti walipokwenda walifanya uamsho wa utawala wa Papa.TK 151.2

    Ili kuwapatia mamlaka makubwa, tangazo la Papa lilitolewa kuanzisha upya Mahakama ya Kanisa Katoliki. Mahakama hii ya kuogofya ilianzishwa na watawala wa Kanisa Katoliki, na mateso ya kutisha yasiyoweza kuvumiliwa mchana yalikuwa yanarudiwa kwenye magereza ya siri chini ya ardhi. Katika nchi nyingi maelfu kwa maelfu ya watu wema na wenye vipawa vya pekee sana wa mataifa, watu wenye akili na elimu kupindukia, waliuawa ama kulazimishwa kukimbilia katika nchi nyingine. (Angalia Kiambatisho)TK 151.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents