Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya 13 - Uholanzi Na Scandinavia

    Kule Uholanzi udikteta wa uPapa ulipata upinzani mapema. Miaka mia saba kabla ya Luther, maaskofu wawili bila woga wowote walionesha kutokuwa na imani na Papa wa Roma. Maaskofu hawa walikuwa wametumwa kama mabalozi kwenda Roma na huko walijifunza tabia halisi ya “utawala wa Papa”: “Umejiingiza mwenyewe kwenye hekalu la Mungu; badala ya kuwa mchungaji, umekuwa mbwa mwitu kwa kondoo.... Ulitakiwa kuwa mtumishi wa watumishi, kama unavyojiita mwenyewe, lakini wewe unajaribu kujifanya bwana wa mabwana...Unayafanya maagizo ya Mungu kudharauliwa.” 149Gerald Brandt, History of the Reformation in and About the Low Countries, bk. 1, p. 6.TK 153.1

    Kame kwa kame wengine waliinuka kutoa mwangwi wa upinzani huu. Biblia ya lugha ya Waldensia ilitafsiriwa aya kwa aya kwenda katika lugha ya Kidachi. Walitangaza “kwamba kulikuwa na faida kubwa ndani yake; hakukuwa na masihara, hadithi za kubuni, wala vitu visivyo na thamani wala udanganyifu, isipokuwa maneno ya kweli.” 150Ibid., p. 14. Hivyo ndivyo walivyoandika marafiki wa imani ya kale, katika kame ya ishirini.TK 153.2

    Mateso yaliyofanywa na Kanisa la Roma yalianza; hata hivyo waumini walikuwa wanazidi kuongezeka, wakisema kuwa Biblia ni mamlaka pekee isiyokosea kidini na kwamba “hakuna mtu atakayelazimishwa kuamini isipokuwa kuongolewa kwa njia ya mahubiri.” 151Martyn, vol. 2, p. 87.TK 153.3

    Mafundisho ya Luther yalipata watu waaminifu na wenye bidii katika kuihubiri Injili nchini Uholanzi. Menno Simons alipata elimu yake kama muumini wa Kanisa Katoliki na aliwekwa wakfu kama padre, hakufahamu lolote kuhusu Biblia na alikuwa ameogopa kuisoma kwa sababu ya hofu ya kuwa mwasi. Alifanya ubadhirifu kutaka kuinyamazisha sauti ya dhamiri yake, lakini bila mafanikio. Baada ya kitambo, aliongozwa kujifunza Agano Jipya; na hili pamoja na Maandiko ya Luther vilimfanya apokee imani ya matengenezo.TK 153.4

    Kitambo kidogo alishuhudia kuuawa kwa mtu aliyekuwa amebatizwa mara nyingine. Hili lilimwongoza kujifunza Biblia kuhusiana na ubatizo wa watoto wadogo. Alijifunza kwamba toba na imani ni masharti ya ubatizo.TK 154.1

    Menno alijiondoa katika Kanisa Katoliki la Roma na kuyatoa maisha yake kufundisha ukweli aliokuwa ameupokea. Kote Ujerumani na Uholanzi kundi la waumini wenye itikadi kali lilikuwa limechipuka, wakivuruga utaratibu na uzuri wa maisha na kuendelea mbele kufanya maasi. Kwa juhudi thabiti Menno aliyapinga mafundisho yao ambayo hayakuwa sahihi na njama za kinyama za watu hao. Kwa miaka ishirini na mitano alikuwa akienda huku na huko katika Uholanzi yote na katika sehemu ya kaskazini mwa Ujerumani akiweka juhudi zenye mvuto uliokuwa unasambaa, akiishi maisha yaliyo kielelezo kulingana na mafundisho aliyokuwa anayatoa. Alikuwa mwaminifu, mnyenyekevu, mwungwana, mkweli, na mwenye bidii. Watu wengi waliongolewa kwa jitihada zake.TK 154.2

    Nchini Ujerumani Charles V alikuwa amepiga marufuku Matengenezo, lakini wana mfalme walikuwa wamesimama kinyume na udikteta wake. Nchini Uholanzi uwezo wake ulikuwa mkubwa. Amri za mateso zilikuwa zinafuatana kwa haraka haraka. Kusoma Biblia, kuisikiliza ikisomwa au kuhubiri, kumwomba Mungu kwa siri, kuachana na kusujudia sanamu, kuimba Zaburi yalikuwa ni makosa ya kuhukumiwa adhabu ya kifo. Maelfu waliangamia mikononi mwa Charles na Philip II.TK 154.3

    Wakati fulani familia nzima ililetwa mbele ya waendesha mashtaka, wakishtakiwa kwa kutoshiriki misa na kufanya ibada zao nyumbani. Kijana mdogo kuliko wote kwenye familia ile alijibu: “Huwa tunapiga magoti na kumwomba Mungu atie nuru kwenye akili zetu na atusamehe dhambi zetu, huwa tunamwombea mfalme wetu, ili ufalme wake upate kustawi na maisha yake yawe yenye furaha; tunawaombea mahakimu wetu ili Mungu awatunze.” Baba wa familia ile na kijana wake mmoja walihukumiwa kufa kwa kuchoma moto kwenye nguzo. 152Wylie, bk. 18, ch. 6.TK 154.4

    Siyo wanaume peke yao lakini wanawake na wanawali walionesha ujasiri usioyumba. “Wake walikuwa wanasimama kando ya nguzo za kuchomea moto waume zao, na wakati mume alipokuwa anauvumilia moto, alikuwa ananong’oneza maneno ya kutia moyo ama kuimba Zaburi kupunguza majonzi yake.” Wanawali walikuwa wanalala kwenye makaburi yao wakiwa hai kana kwamba walikuwa wanaingia vyumbani mwao kulala wakati wa usiku, ama kwenda kwenye majukwaa ya moto ya kuchomea watu na mavazi yao yaliyo mazuri sana ka na kwamba walikuwa wanakwenda kwenye arusi zao.” 153Ibid.TK 155.1

    Mateso yalikuwa yanaongeza idadi ya mashahidi wa ukweli. Mwaka baada ya mwaka mfalme alikuwa anaendeleza kazi yake ya ukatili, lakini bila mafanikio. Hatimaye William wa Orange aliruhusu uhuru wa kumwabudu Mungu huko Uholanzi.TK 155.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents