Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Uvumilivu wa Mungu

    Bwana alichelewesha hukumu zake kwa takriban miaka arobaini. Bado kulikuwa na Wayahudi wengi ambao walikuwa hawajui tabia na kazi ya Kristo. Watoto walikuwa hawajaiona nuru ambayo wazazi wao walikuwa wameikataa. Kwa njia ya mahubiri ya mitume, Mungu alifanya nuru hiyo iwaangazie. Waone jinsi unabii ulivyokuwa umetimia, siyo tu katika kuzaliwa kwa Kristo na maisha yake, bali pia katika kufa na kufufuka kwake. Watoto hawakuhukumiwa kwa sababu ya dhambi za wazazi wao; lakini walipoikataa nuru ya ziada waliyokuwa wamepewa, walikuwa washirika wa dhambi za wazazi wao na kukijaza kipimo cha uovu wao.TK 24.2

    Wayahudi waliikataa fursa ya mwisho ya rehema kwa tabia yao sugu ya kutokuwa na toba. Mungu akawaondolea ulinzi wake. Taifa likaachwa chini ya utawala wa kiongozi waliyekuwa wamemchagua. Shetani akaamsha tamaa mbaya katika mioyo. Watu wakafanya mambo bila kutafakari—wakitawaliwa na tamaa, hasira kali, wakawa wakatili kama Shetani. Marafiki na ndugu wakawa wanasalitiana. Wazazi wakawa wanaua watoto wao, na watoto wakawa wanaua wazazi wao. Watawala wakawa hawana uwezo wa kujitawala wenyewe. Hamaki ziliwafanya kuwa watawala dhalimu. Wayahudi walikuwa wamekubali ushuhuda wa uongo kumhukumu Mwana wa Mungu asiye na hatia. Sasa mashtaka yasiyo ya kweli yakafanya maisha yao kuwa ya mashaka. Hofu ya Mungu ilikuwa haiwasumbui tena. Shetani alikuwa analiongoza taifa lao.TK 24.3

    Viongozi wa vikundi vilivyokuwa vinapingana walishambulia majeshi ya wapinzani wao na kuua bila huruma. Hata utakatifu wa hekalu haukuzuia ukatili wa kutisha. Hekalu lilinajisiwa kwa miili ya waliouawa. Licha ya hayo, wachochezi wa mambo haya ya kutisha walikuwa wanadai kuwa walikuwa hawana wasiwasi wa kuangamizwa kwa Yerusalemu, kwani ulikuwa mji wa Mungu. Hata wakati majeshi ya Kirumi yanalizingira hekalu, wengi walikuwa wanaamini kuwa Aliye juu angeingilia na kuwashinda maadui zao. Lakini Israeli ilikuwa imeukataa ulinzi wa Mungu, na sasa ilikuwa haina ulinzi.TK 24.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents