Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Wesley Anusurika Kifo

    Watu waliokuwa na mvuto walitumia uwezo dhidi yao. Wachungaji wengi walikuwa wamewachukia na milango ya makanisa ilikuwa imefungwa dhidi ya imani safi. Katika mimbari zao, wachungaji waliwakana hadharani wakionesha dalili za udhalimu na uovu. Mara kwa mara Wesley alinusurika kuuawa kwa mwujiza wa neema ya Mungu. Ilipoonekana hapakuwa na namna ya kuokoka, malaika katika umbo la binadamu alisimama upande wake na kundi la wahalifu walikuwa wanaanguka na mtumishi Wakristo alikuwa anapita kwa usalama kutoka katika hatari hiyo.TK 167.4

    Kuokolewa kwake kutoka katika moja ya matukio haya, Wesley alisema: ‘ingawaje wengi walikuwa wanajaribu kwa bidii kukamata ukosi wa mavazi yangu ili kuniangusha chini, hawakufaulu kabisa: ni mmoja tu aliwahi kukamata kwa nguvu upindo wa kizibao changu, ambacho upesi kilibakia mkononi mwake, na mwingine alipokamata upindo katika mfuko ninaohifadhia fedha, nilichoropoka mfuko ukawa umetatuka tu kidogo....Mtu mwenye nguvu aliyekuwa nyuma yangu, alijaribu mara kadhaa kunipiga kwa fimbo kubwa ya mwaloni; ambayo iwapo ingenipata kisogoni kwangu ningekufa. Kila wakati pigo lake liligeuziwa upande mwingine, sikuelewa ilikuwa inatokeaje, kwa sababu sikuweza kujisogeza upande wa kuume ama wa kushoto.” 166John Wesley, Wrks, vol. 3, pp.297, 298. TK 168.1

    Wamethodisti wa kipindi hicho walikuwa wanavumilia dhihaka na mateso, na mara nyingi walikuwa wanavumilia vurugu pia. Mara nyingine, mathalani; matangazo yaliwekwa katika mbao za matangazo za umma yakiwaita kwa pamoja wale wote waliokuwa wanahitaji kwenda kuvunja kwenye madirisha ya Wamethodisti na kuwaibia kukusanyika mahali na kwa muda fulani. Mateso yaliyokuwa yanaendeshwa kwa mpangilio yalikuwa yanafanywa dhidi ya watu ambao kosa lao peke yake lilikuwa kuwageuza wenye dhambi kuelekea njia ya utakatifii.TK 168.2

    Kumomonyoka kwa hali ya kiroho nchini Uingereza muda mfupi kabla ya wakati wa Wesley kwa kiasi kikubwa yalikuwa ni matokeo ya fundisho kuWakristo alikuwa ameifuta kabisa sheria ya maadili na kwamba Wakristo hawalazimiki tena kuitunza. Wengine walikuwa wanadai kuwa halikuwa jambo la lazima kwa wachungaji kuwashawishi watu kutii maagizo ya sheria hiyo, kwa kuwa wale waliokuwa wamechaguliwa na Mungu kuokolewa “watakuwa wanaongozwa na kicho na wema wao kwa Mungu” na wale waliokuwa wamepangiwa kuangamia milele “hawakuwa na uwezo wa kuitii sheria ya Mungu.”TK 168.3

    Wengine walikuwa wanadai kuwa “wateule hawawezi kuanguka na kuiacha neema ama kupoteza kukubaliwa kwao na Mungu,” na hata kufikia hitimisho lenye kuchafua moyo sana kwamba “matendo wanayotenda waovu kwa kweli siyo maovu kiasi hicho... kwa sababu hakutakuwa na wasaa wa kuungama dhambi zao ama kuziacha kwa kutubu” 167McClintock & Strong, Cyclopedia, art. “Antinomians.” Kwa hiyo, walikuwa wanadai kwamba, “hata kwa dhambi zenye kuaibisha mno” zilizokuwa zinajulikana pote kuwa ni uvunjifu mkubwa wa sheria ya Mungu haikuwa dhambi mbele za Mungu” kama zingekuwa zimetendwa na mteule. “Hawawezi kufanya lolote linalomchukiza Mungu ama lolote linalokatazwa na sheria.”TK 168.4

    Mafundisho haya mabovu na ya kuogofya kimsingi yanafanana na yaliyotangulia yenye kufundisha kuwa hakuna sheria ya Mungu isiyoweza kubadilishwa kama kiwango cha haki na kwamba maadili yanadhihirishwa na jamii yenyewe na kila mara yalikuwa yanabadilika. Dhana hizi zote huwa zinaongozwa na yule aliyekuwa miongoni mwa wakazi wa mbinguni wasio na dhambi aliyeanzisha kazi ya kuvunja vizuizi vya haki vya sheria ya Mungu.TK 169.1

    Fundisho la maagizo ya Mungu, yasiyobadilika yanayotengeneza tabia za wanadamu, limewaongoza wengi kuikataa sheria ya Mungu. Na kwa uthabiti Wesley alikuwa analipinga fundisho hili lililopelekea baadhi ya Wakristo kudhani kuwa neema ya Mungu inawapa watu uhuru wa kutozishika sheria za maadili. “Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa.” “...Mungu Mwokozi wetu...ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli. Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, MwanadamUkristo Yesu; ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote.” “Kristo “nuru halisi,...amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu.” Tito 2:11; lTim. 2:3-6; Yn. 1:9. Watu hujikosesha wenyewe wokovu kwa sababu ya kukataa kwa hiari yao karama ya uzima.TK 169.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents