Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  John Knox

  Hamilton, Wishart na wengine wengi sana, watu wanyenyekevu na wenye imani walimalizia maisha yao motoni. Lakini kutokana na kuchomwa moto kwa Wishart alitokea mtu ambaye asingewezekana kunyamazishwa na ndimi za moto, mtu ambaye chini ya uongozi wa Mungu atapiga pigo la mauti kwa udhalimu wa papa katika Uskochi.TU 116.3

  John Knox alitupilia mbali mapokeo ya kansia apate kujulisha kwa neno la Mungu. Mafundisho ya Wishart yalimsaidia kukata shauri la kuachana na Rumi, na kuambatana na watengenezaji.TU 116.4

  Akisukumwa na rafiki zake ili ahubiri alishinda kwa kuona jinsi hiyo ilivyo nzito. Palikuwa na mashindano makuu ndani yake, na hofu nyingi ikijaribu kubeba madaraka hayo ya kuhubiri, lakini mwishowe alishinda woga, akaanza kuhubiri, wala hakuogopa nyuso za watu. Alipokutana na malkia wa Uskochi, John Knox hakushawishika na lolote, wala hakutishika na chochote. Aliwafundisha watu kuamini dini hiyo ya matengenezo, ingawa ilipigwa marukufu na serikali. Malkia alimwambia kuwa kufundisha watu kushika dini hiyo ni kinyume, tena ni kuasi amri za Mungu. Knox akajibu kishujaa: “Kama watu wote wa uzao wa ibrahimu wangekuwa na dini ya Farao wangalikuwa raia wa nani mheshimiwa? Tena kungalikuwa na dini gani ulimwenguni? Au kama watu wote wa siku za mitume wangalikuwa na dini ya Warumi (serikali) kungalikuwa na dini gani ulimwenguni?”TU 116.5

  Malkia Mary Akasema, “Ninyi mnatafsiri maandiko kwa namna moja na Warumi wanatafsiri kwa namna nyingine, sasa nitamwamini nani na mwenye ukweli ni nani?”TU 117.1

  Knox akajibu “Utamwamini Mungu, ndivyo neno lake lisemavyo dhahiri. Neno la Mungu ni dhahiri, wala halina siri na ikionekana sehemu isiyoeleweka Roho Mtkatibu ambaye hana kinyume, hueleza mambo yale wazi kabisa mahali pengine katika Maandiko”TU 117.2

  Knox akiwa na ujasiri, bila kuhofia hata maisha yake kutoka katika ukafiri wa Rumi Katika Uingereza kusimamishwa kwa dini ya Kiprotestant kama dini ya Taifa kulipungua sana, lakini hakukumalizika kabisa. Kawaida za Kirumi za ibada ziliendelea kuwako. Utawala wa papa ulikataliwa kuwa juu ya mambo ya dini, lakini badala yake mfalme akakubaliwa kuwa mtu wa kanisa pia. Mpaka wakati huo kulikuwa na machafuko makubwa kuhusu Injili. Uhuru wa dini haukuwepo: ingawa ukatili wa Kirumi ulikuwa umekoma, haukuendelezwa na Waprotestant, walakini uhuru wa kila mtu kuabudu apendavyo haukuwapo. Wapinzani waliendelea kuteseka kwa miaka mingi.TU 117.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents