Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Wesley Aponyoka Kifo

  Watu mashuhuri walitumika kuwapinga wahubiri hao. Walionyesha hali ya kiuadui sana, na hawakuwapa nafasi ya kuhubiri makanisani. Kwahiyo ukweli wa neno la Mungu ukafungiwa nje. Watu hao waliwalaumu wazazi katika mikutano ya hadhara. Hivyo wakaongeza hali ya giza nene nchini. Kwa hali hiyo maisha ya Wesley yalikuwa hatarini kila mara. Wakati fulani John Wesley aliepuka kifo kwa mwujiza wa Mungu. Alipozingirwa na kundi la watu waovu na ikaonekana kuwa hakuna njia ya kuokoka, Malaika akiwa na umbo la binadamu akawafukuza watu hao, na Wesley akapita salama, katika hatari hiyo.TU 120.5

  Katika habari za kuokoka kwa Wesley alisema “Ijapokuwa majaribio mengi ya kuninasa yamefanyika, hayakufaulu, ingawa moja lilikaribia kuninasa. Mkorofi mmoja alinipiga mara nyingi akanijia kwa nyuma, akitumia fimbo, ambayo mara kama angenipiga kichwani kazi yake ingakamilika. Kila mara kipigo kilinikosa bila sababu, kwa sababu sikujaribu kukwepa hata kidogo.” Wakristo wa Methodist wa siku hizo walivumili mateso na kufanyiwa mizaha, na kutendewa ukatili. Wakati mwingine tangazo lilitolea kwamba, wale wanaotaka kushambulia wakristo wa Methodist wakakutane mahali fulani na saa fulani. Mateso ya kuendelea yaliwahusu wale wanaowaongoa watu toka katika upotevu, na kuwaleta nuruni.TU 121.1

  Upotovu wa kiroho katika Uingereza kabla ya siku za Wesley, ulikuwa matokeo ya mafundisho maovu ya kwamba, eti Kristo aliiondoa sheria ya amri kumi, na ya kwamba hakuna haja ya kuzishika. Wachungaji wengine waliwaambia wakristo wao kuwa kuzitii amri hizo ni kupoteza wakati tu, kwa maana wale Mungu aliowachagulia uzima waatadumu watakatifu daima, na wale Mungu aliowapangia kufa, hata wafanyeje wasingefaulu.TU 121.2

  Wengine tena walishikilia imani kwamba wateule wasingeweza kufanya dhambi, na ya kwamba waovu ni waovu tu milele, wasingeweza kubadilika wala kutubu, wamevuka mpaka wa rehema. Hata walithubutu kusema kuwa kuvunja sheria ya Mungu siyo dhambi, kama tendo hilo lingetendwa na mteule yeyote.TU 121.3

  Mafundisho haya machafu ni sawa na mafundisho yaliyotokea baadaye yasemayo kuwa hakuna sheria yoyote ya Mungu isiyobadilika ambayo ndiyo kipimo cha kuongoza mambo yote; lakini sheria yoyote huweza kubadilishwa na watu ili ifuatane na hali yao. Mambo haya yote hutokana na yule aliyeanzisha uasi katika viumbe vya mbinguni visivyo na dambi, na kujaribu kuvunja amri ya Mungu isiyovunjika.TU 121.4

  Mafundisho ya mbinguni ni kwamba, sheria ya Mungu ni ya milele, haibadiliki ambayo watu wameikataa na kumkataa Mungu pia. Weslye aliyapinga mafundisho hayo maovu. “Neema ya Mungu iletayo wokovu, imefunuliwa kwa watu wote” Mungu mwokozi wetu “…anataka watu wote waokolewe, na kuufikia ujuzi wa kweli. Maana Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu ana wanadamu. Mwanadamu Yesu Kristo aliyejitoa kuwa fidia ya wote” “Kristo, nuru inayomwangazia kila mtu ajaye ulimwenguni” Tito 2:11; 1Tim. 2:3-6; Yohana1:9 Watu waliukosa wokovu kwa kukataa kupokea kipawa cha uzima.TU 122.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents