Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Jinsi Ingalipasa Kuwa

  Kule kukimbilia kwa Wahunguenots kutoka Ufaransa kulileta upungufu mkubwa sana nchini. Miji iliyokuwa ikistawi kwa wingi wa viwanda ilibakia kuwa magofu ya kutu…. Imekadiriwa kuwa wakati wa mapinduzi kulikuwako maskini laki mbili katika mji wa Paris waliokuwa wakilishwa na kusaidiwa na mfalme. Waliokuwa na mafanikio katika taifa zima ni wa Jesuits peke yao. Wengine wote walikuwa wamenyauka.TU 131.1

  Injili peke yake ingetatua matatizo yaliyoipata nchi ya Ufaransa, ambayo yaliwafadhaisha waongozi wa serikali, na wadini, wafalme na mwisho kuliangamiza taifa zima. Lakini chini ya uongozi wa kanisa la Rumi watu wamepoteza mafundisho ya Kristo yahusuyo kujikana nafsi, na kutoa huduma isiyokuwa na ubinafsi kwa wahitaji. Matajiri hawakuwa na shughuli kwa maskini. Choyo cha kujitajirisha kilizidisha hali ya maisha kuwa ya matatizo makubwa. Kwa karne na karne hapakuwa na maafikiano baina ya matajiri na maskini. Matajiri waliwaonea maskini, na maskini waliwachukia matajiri.TU 131.2

  Katika mikoa mingi wakulima wa hali ya chini waliishi kwa rehema za makabaila, nao walilazimishwa kutii na kufuata kama vile mabwana wanavyotaka. Walitozwa kodi kubwa sana na watawala na makasisi.TU 131.3

  Wakulima walikuwa nusura kufa njaa kwa vile wakubwa wao walivyowaonea. Maisha ya kilimo hayakuwa na pumziko la aina yoyote, na ya ufukara kabisa….. Malalamiko yao …. Yalihesabiwa kuwa ni ujeuri, wala hayakujaliwa. Rushwa ilienea, hata mahakamani ilijaa tele. Kodi iliyotozwa kwa watu, haikuingia katika hazina ya serikali, hata nusu yake. Karibu yote ilipita katika mikono ya wapenda mali, ambao ni watumishi wa serikali. Kodi hiyo iliyotozwa kwa wingi hivyo, wale watumishi wao hawakuhusika na utoaji huo, ila tu raia wa kawaida. Wale waliongoja kunyakua na kujinufaisha. Ufedhuli ulikuwa hausemeki.TU 131.4

  Kwa muda wa zaidi ya nusu karne kabla ya mapinduzi utawala ulikuwa mikononi mwa Lois XV, mfalme aliyejidhihirisha kuwa mtu mlegevu, apendaye uasherati. Kifedha aliisumbua sana serikali na kuitia katika matatizo, na kukasirisha raia mno, hata hapakutakiwa kuwa na nabii wa kutabiri maafa yatakayotokea karibu, maana mambo hayo yalijitangaza yenyewe. Walijaribu kurekebisha mambo, lakini ilikuwa kazi bure. Ajali iliyokuwa inakabili Ufaransa ilionekana kwa maneno ya mfalme, aliyosema, “Baada yangu, ndipo uharibifu utatokea”TU 131.5

  Rumi ilikuwa imewashawishi watawala wa Ufaransa wawafungie watu gizani kwa kutopata nuru ya Neno la Mungu, ikiazimu kuwafunga wote watawala na raia katika giza la kutopata neno la Mungu. Hatari mbaya zaidi ya ile ya kuangamia kimwili ilikuwa uharibifu wa kiroho. Kuwanyima watu Biblia, na kuwaacha gizani kuliwafanya wazame katika ufasiki na uovu mpaka wakawa hawafai kujitawala.TU 131.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents