Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  2/Wakristo wa Kwanza Waaminifu wa Kweli

  Yesu aliwafunulia wanafunzi wake hali ya watu wake jinsi itakavyokuwa tangu siku ile atakayoaacha kwenda zake mbinguni, hata siku atakaporudi mara ya pili kwa nguvu na utukufu mwingi. Alipenyeza macho yake akaona hali ya fujo na mateso itakayowapata wafuasi wake siku za usoni. Soma Mathayo 24:9,21-22. Wafuasi wa Kristo hawana budi kupitia njia ile ile ya dharau na dhihaka na masumbuko, kwa Mwokozi wa ulimwengu, utaonekana kwa wote watakaoliamini jina lake pia.TU 9.1

  Umizimu uliona kuwa kama ukristo utafaulu utaondolea mbali mahekalu na madhehebu zote za giza kwa hiyo moto wa mateso ukachochewa. Wakristo walinyang'anywa mali zao, na kufukuziwa mbali kutoka katika miji yao. Watu wenye elimu na wasio na elimu, walichinjwa bila huruma.TU 9.2

  Mateso yalianzia wakati wa mfalme Nero yakaendelea kwa karne nyingi. Wakristo walisingiziwa kuwa ndio wameleta njaa, tauni, na tetemeko la nchi. Walisaliti na wachochezi walikuwa tayari kusaliti na kuwasingizia wasio na hatia kwamba ni hatari kwa jamii. Wengi sana walitupwa katika matundu ya wanyama wakali au walichomwa moto; wengine walitundikwa mitini, wengine walivishwa ngozi za wanyama wakatupiwa mbwa na kurarulia nao. Katika mikutano ya hadhara, watu wengi walihudhuria ili kushangilia mateso yao na jinsi walivyokufa kikatili kabisa.TU 9.3

  Wafuasi wa Kristo walilazimishwa kutafuta maficho mahali pa ukiwa nyikani. Chini ya milima iliyoko nje ya mji wa Rumi walichimba mifereji mirefu, wakafanya makao katika mapango hayo chini ya miamba. Humo ndimo walimozika wafu wao pia. Hayo yalikuwa makimbilio yao. Wengine walikumbuka maneno ya Bwana, kwa hiyo walipoudhiwa walifurahi tu. “Thawabu yao itakuwa kubwa sana mbinguni, maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yao” Mathayo 5:11-12.TU 9.4

  Nyimbo za ushindi zilisikika kutoka katika miale ya moto wakiziimba kwa furaha. Kwa imani walimwona Kristo na malaika wakiwazunguka kwa kupendezwa sana kwa ajili ya ushujaa wao. Sauti ilisikika kutoka katika kiti cha enzi cha Mungu, ikisema: “Uwe mwaminifu mpaka kufa, nami nitakupa taji ya uzima”. Ufunuo 2:10.TU 10.1

  Shetani alijitahidi kuliharibu kanisa la Kristo, kwa njia ya mateso, lakini ilikuwa kazi bure. Watendakazi wa Mungu walichinjwa, lakini Injili ilizidi kuenea, na wafuasi kuongezeka. Mkristo mmoja alisema, “Mnatukatakata kama majani, lakini tunazidi kuongezeka; damu ya wakristo ndiyo mbegu.”TU 10.2

  Kwa hiyo shetani alipanga vita kwa njia nyingine ya kufaulu zaidi. Alisimamisha bendera yake katika kanisa la kikristo, ili kupata wakristo wadanganyifu, wenye hila, hivyo alifaulu kuliko alivyotumia mateso, akatumia vishawishi na heshima. Ibada ya Sanamu ilikubaliwa kuwa ni sehemu ya ukristo, na ukweli halisi akakataliwa. Walijidai kuwa watu wa Mungu lakini huku wakishikilia dhambi, bila kuwa na haja ya kuziungama na kuziacha. Hapakuwako badiliko lolote katika mioyo yao. Walikubaliana tu ya kuwa wote “waamini katika Kristo”TU 10.3

  Sasa kanisa lilikuwa katika hatari kubwa. Magereza, mateso, kuchomwa moto na upanga, hayo yote yalikuwa nyeti kulinganisha na hali hii ya ukristo bandia. Baadhi ya wakristo walisimama imara. Wengine walipendelea kugeuza imani zao na kufuata ukristo huu bandia. Katika vazi hili jipya la ukristo wa kujifanya, shetani alijipenyeza kanisani na kuchafua imani yao.TU 10.4

  Wakristo wengi baadaye walipotoka kabisa na kushusha hadhi yao. Mwisho mwungano wa ukristo na umizimu ulifanyika. Ingawa waabudu sanamu walijidai kuungana na kanisa, lakini walishikilia sanamu zao tu, ila walibadili sanamu zao ziwe mfano wa Yesu, na mfano wa Maria na watakatifu wengine. Wakaingiza mafundisho ya uongo mambo ya ushirikina na uchawi, na mambo ya ibada ya sanamu. Hivyo vyote vikawa sehemu ya imani na ibada ya ukristo. Kwa hiyo ukristo halisi ukachafuliwa sana, na kanisa likapoteza hadhi yake na uwezo wake. Walakini wengine hawakupotoshwa. Walishikilia kanuni yao ya imani ya kweli.TU 10.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents