Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Matokeo ya Kuvuna Damuni

  Rumi badala ya kuwashikilia watu katika hali ya ujinga wa kukubali tu mambo bila kuwaza, na kuwafuatafuata tu mambo ya Rumi, watu wakawa wakafiri waliojanjaruka na kuwa waasi. Wakadharau mafundisho ya Rumi na kuyaona mkatili na mwonevu, kwa hiyo hawakutaka kujihusisha naye. Wakadhani kuwa hayo ndiyo matokeo ya Biblia kama inavyofundishwa na Rumi.TU 132.1

  Warumi wamemwakilisha Mungu vibaya mbele za watu, na sasa matokeo yake yamekuwa kuikataa Biblia na mwenye Biblia. Katika hali hiyo Voltaire na wafuasi wenzake wakaiasi Biblia kabisa, wakaueneza ukafiri tu. Rumi imewafunga watu chini ya mongozi yake, na sasa watu walitupilia mbali mambo yote ya Rumi. Kwa chuki hiyo wakakataa mambo yote ya uongo na ya kweli pia.TU 132.2

  Walipoanza mapinduzi kwa ukubali wa mfalme watu walipata wawakilishi wengi zaidi kuliko wakuu wa kila hali. Kwa hiyo walikuwa na uwezo mwingi zaidi. Lakini walikuwa hawajui jinsi ya kutumia uwezo huo kiakili. Wakawa wenye kuonea na kudhulumu watu. Halafu watu wakaazimia kujipigania na kulipa kisasi. Walioonewa wakawageukia waliowaonea.TU 132.3

  Ufaransa ilivuna mavuno katika damu kwa matokeo ya kuyakubali mambo ya Rumi. Pale Ufaransa ilipoanzia kuchoma watengenezaji ikiongozwa na Rumi, ndipo pale pale mashine za kukata vichwa zilipowekwa ili kukata vichwa vya wakuu wakati wa mapinduzi. Mahali pale mfia dini wa kwanza wa Kiprotestanti alipofia katika karne ya kumi na sita, ndipo pale mtu wa kwanza allipokatwa kichwa wakati wa mapinduzi katika karne ya kumi na nane. Wakati hifadhi ya sheria ya Mungu ilipotupiliwa mbali, taifa zima liliasi, na nchi yote ikiwa yenye machafuko ya kuuana ovyo. Vita ya kupigana na Biblia inajulikana kama utawala wa kitisho katika ulimwengu. Mshindi wa leo, kesho atahukumiwa.TU 132.4

  Mfalme, kiongozi wa dini, wakuu wa serikali, wote walilazimika kutii na kufuata amri za watu waliochafuka mawazoni na kuwa kama wenda wazimu. Wale waliotangaza kifo cha mfalme walimfuata pia kwa kumnyonga. Machinjano yalikuwa mengi sana. Watu wote wliodhaniwa kuwa hawayaungi mkono mapinduzi walichinjwa ovyo. Ufaransa ikawa mbuga ya majeshi ya watu wasio na utaratibu, wakizunguka zunguka na kuchijana. Katika mji wa Paris machafuko yalikuwa yakifuatana mfululizo, na raia waligawanyika katika vikundi vya usaliti; visivyokuwa na jambo la kufanya ila kuzungukazunguka tu na kufanya ghasia …… Nchi ilikuwa karibu kufilisika, jeshi la askari ililikuwa likifanya ghasia, likidai mishahara ya nyuma ambayo haikulipwa. Watu katika mitaa walikuwa shidani kukosa chakula, mikoani kulijaa maharamia ambao walipora kila kitu kilichoonekana, na ustaarabu ulikuwa katika ukingo wa kutoweka kwa ajili ya fujo na ghasia zilizoenea kila mahali bila mtu wa kuzikomesha.TU 132.5

  Sasa watu walikuwa wamejifunza mafundisho ya ukatili na mateso ambayo Rumi imewafundisha kwa bidii, Sasa watu waliokamatwa na kuchomwa moto sio wanafunzi wa Yesu Kristo. Wanafunzi wa Yesu walichomwa zamani, na wengine walifukuzwa nchini zamani. Wakati huu mapadri wa Rumi na mfuasi wa Rumi ndiyo wanaouawa. Magereza yaliyojaa Wahuguenots zamani, sasa yalijaa watesi wao. Mateso yote ya kila namna ambayo kanisa la Roman Katoliki iliwatesa wafuasi wa Kristo ambao waliitwa wazushi, yamewageukia waongozi wa Rumi.TU 133.1

  Halafu zikafika siku…. Ambapo majasusi walienea kila mahali wakivizia wahusika; wakati mashine za kunyongea watu zilikuwa hazitulii; wakati magereza yalijaa watu kama merikebu iliyopakia watumwa; wakati damu za watu zilitiririka katika mto wa Saine…. Mistari mirefu ya wafungwa ilikatwakatwa na marisasi. Matundu yalifanywa chini ya mashua zilizojaa watu... Hesabu ya wavulana na wasichana wa umri wa miaka kumi na saba waliochinjwa kwa ajili ya kupinga serikali ni mamia na mamia. Watoto wachanga walinyakuliwa kutoka kwa mama zao na kuchomwa mikuki popote walipokutwa.TU 133.2

  Haya yote yalikuwa matakwa ya Shetani. Kampuni yake ni udanganyifu, na kusudi lake ni kuangamiza watu, ili kuchafua kazi ya Mungu na kuvuruga mpango wa upendo, ili kuleta huzuni mbinguni. Halafu kwa njia ya udanganyifu wa kihila atupe lawama zote kwa Mungu. Ndivyo anavyowaongoza watu waamini, kana kwamba ndivyo Mungu alivyopenda. Watu walipougundua udanganyifu wa Warumi, shetani akiwaongoza waamini kuwa dini yote ni udanganyifu mtupu, na Biblia ni hadithi tupu za uongo.TU 133.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents