Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kosa Baya Kuliko Yote

  Kosa baya mno lililosababisha maafa mabaya katika Ufaransa lilikuwa kutojali ukweli mkuu: uhuru wa kweli umo katika kulitii Neno la Mungu. Lakini kulikataza au kulipinga marufuku hukaribisha maafa. “Laiti ungalisikiliza amri zangu! Ndipo amani yako ingalikuwa kama mto wa maji, na haki yako kama mawimbi ya bahari”. Isaya 48:18. Wote ambao hawajifunzi fundisho katika kitabu cha Mungu wanaagizwa wajifunze kutokana na historia.TU 134.1

  Wakati shetani alipolitumia kanisa la rumi liwaongoze watu waziasi amri za Mungu, kazi yake ilikuwa najisi. Kwa kazi ya roho ya Mungu, kazi ya shetani ilizuilika isifikie maazimio yake. Watu hawakufuatia asili ya maafa yao, na kugundua kiini chake. Lakini wakati wa mapinduzi sheria ya Mungu ilikataliwa dhahiri na bunge la taifa. Na wakati wa utawala wa kitisho uliofuta, watu waliona asili yake.TU 134.2

  Uasi wa sheria ya kweli na haki lazima matokeo yake yawe uangamivu. Roho ya Mungu inayozuia ukatili wa shetani ilikuwa ikiondelewa kwa sehemu kubwa, kwa hiyo mtu yoyote aliyetaka kutenda matendo ya ukatili kwa wenzake hakuwa na kizuizi. Watu hawakufuatia asili ya maafa yao, na kugundua kiini chake. Lakini watu wa mapinduzi sheria ya Mungu ilikataliwa dhahiri na bunge la taifa. Na wakati wa utawala wa kitisho uliofuata, watu waliona asili yake.TU 134.3

  Uasi wa sheria ya kweli ya haki lazima matokeo yake yawe uangamivu. Roho ya Mungu inayozuia ukatili wa shetani ilikuwa ikiondolewa kwa sehemu kubwa, kwa hiyo mtu yeyote aliyetaka kutenda matendo ya ukatili kwa wenzake hakuwa na kizuizi. Watu waliochagua kuasi, basi walivuna mavuno yake. Nchi ilijaa uharamia na uasi wa kila hali. Maombolezo ya uchungu yalisikika kote, tangu mijini mpaka mashambani kwa ajili ya maharamia walikuwa wakiharibu vitu popote. Ufaransa ilitikiswa kana kwamba imekumbwa na tetemeko la nchi. Dini, sheria, uhuru na utulivu, jamaa, serikali na kanisa, vyote vilivurugwa kabisa na wafedhuli ambao wameelekezwa kuikana sheria ya Mungu.TU 134.4

  Mashahidi wa Mungu waliochinjwa na wenye kukufuru “watokao katika shimo la abuso”. Hawatakaa kimya daima. “Na baada ya siku hizo tatu u nusu roho ya uhai itokayo kwa Mungu ikawaingia, wakasimama juu ya miguu yao; na hofu kuu ikawaangukia watu waliowatazama” ufunuo 11:11. Mwaka 1793 sheria ilipitishwa na bunge la ufaransa ya kupiga marufuku Biblia. Baada ya miaka mitatu na nusu tangu sheria hiyo ipitishwe, bunge lile lile lilikutana na kufuta sheria hiyo. Watu walitambua kuwa imani kwa Mungu ndiyo msingi wa maadili na wema.TU 134.5

  Kuhusu Mashahidi wawili, agano la kale na Agano Jipya nabii husema zaidi kuwa “Wakasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikiwaambia, Pandeni hata huku. Wakapanda mbinguni katika mawingu adui zao wakiwatazama” Ufunuo 11:12. Mashahidi wawili wa Mungu wameheshimiwa kwa namna ambayo haijaonekana. Katika mwaka 1804 chama cha kupiga chapa Biblia, yaani British and Foireign Bible Society kiliundwa, kikifuatiwa na mashirika mengine yaliyoundwa barani Ulaya. Mwaka 1816 Chama cha Kimarekani cha Biblia kilianzishwa. Tangu hapo Biblia ilitafsiriwa katika lugha mamia, nzima au sehemu.TU 134.6

  Kabla ya mwaka 1792 kazi za misheni zilijaliwa kidogo sana. Lakini katika mwisho wa karne ya kumi na nane mageuko makuu yalitokea. Watu hawakuridhika na maongozi ya kibinadamu tu ila waliona haja ya maongozi ya Mungu; ambayo hupatikana kwa dini. Tangu wakati huo kazi za misheni zimekuwa na kuendelea kiajabu.TU 135.1

  Maendeleo katika uchapaji husukuma mbele kazi ya kueneza Biblia kwa namna ya pekee. Kuvunjilia mbali chuki za kitaifa ambayo ni hali ya zamani, na kuondolewa mbali uwezo wa makasisi wa Rumi, kumefungua njia ya kuliingiza Neno la Mungu pale lilipozuiliwa zamani. Sasa Biblia imefika pande zote za dunia.TU 135.2

  Kafiri mmoja Voltaire alisema “Nashangaa kusikia kuwa watu kumi na wawili ndio walioimarisha dini ya Kikristo. Nathibitisha kwamba mtu mmoja atosha kuifuta.” Watu mamilioni walijiunga kupinga Biblia, lakini iliwashinda. Kama wakati wa Voltare palikuwa na Biblia mia moja, basi kuna malaki ya vitabu hivo sasa hivi. Kwa maneno ya watengenezaji wa zamani “Biblia ni fuawe lililochakaza nyundo nyingi” Chochote kilichojengeka kwa msingi ya kibinadamu, kitaangamia lakini kilichojengeka Mwambani, ambao ni neno la Mungu kitadumu milele.TU 135.3

  Marejeo: TU 135.4

  Blackwood Magazine, November 1870 TU 135.5

  Sir. Walter Scott, Life of Napoleon, Vol. 1 ch. 17 TU 135.6

  Wylie, bk. 22, ch. 7 TU 135.7

  Henry White the massacre of St. Bartholomew, ch. 14 p. 34 TU 135.8

  Scott, Vol. 1 ch. 17 TU 135.9

  Lacretele History Vol. II p. 309 in Sir Archibad Alison History of Europe, Vol. ch. 10 TU 135.10

  Scott Vol. 1 ch. 17 TU 135.11

  M. A Thiers, History of the French Revolution, Vol. 2 p. 370 -371. TU 135.12

  D' Aubigne, History of Reformation in Europe in the Time of Calvin, bk. 2 ch. 36. TU 135.13

  Wlie, bk. 13 ch. 20 TU 135.14

  Ibid.TU 135.15

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents