Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Tetemeko Lililotikisa Ulimwengu

  Katika kutimiza unabii huo kulitokea tetemeko kuu la nchi katika mwaka 1755. Hilo lilizidi matetemeko yote yaliyotangulia. Linajulikana kama tetemeko la Lisbon. Lilienea ulaya, Afrika na Marekani. Tetemeko hilo lilisikika katika nchi za Greenland, West Idies, Madeira, Norway, Sweden, Uingereza na Ireland. Lilienea katika umbali wa maili za mraba miliioni nne. Katika Afrika mtikiso wa ardhi ulikuwa wa nguvu sawa na ule wa Ulaya. Sehemu kubwa ya mji wa Algiers uliharibiwa. Wimbi kuu la maji lilifurikisha mji wa Algiers uliharibiwa. Wimbi kuu la maji lilifurikisha miji ya Hispania na ya Afrika. Milima ya Ureno, ambayo ni mikubwa ilitikishwa kwa nguvu sana hata ikawa kana kwamba inang'olewa, mingine ilipasuka kileleni kwa ajabu. Udongo kutoka milimani ulitiririka na kujaza mabonde. Miali ya moto ilionekana katika milima hiyo.TU 143.1

  Katika mji wa Lisbon, ngurumo ya radi ilisikika ndani ya ardhi, baada ya muda kidogo mtetemo wa nguvu sana uliangamiza sehemu kubwa ya mji. Katika tetemeko hilo ambalo lilidumu muda wa dakika sita hivi, watu sitini elfu waliangamia. Bahari kwanza ilikuwa kana kwamba inakupwa, na kuacha nchi kavu, halafu ilirudi kwa nguvu ikigharikisha vitu. Iliinuka juu zaidi ya futi hamsini kuliko kawaida yake. Yalikuwa yamejaa watu wakiabudu. Katika hao na wachache sana waliopona. Hofu na vilio vya watu vilizidi kiasi, hata haielezeki. Maombolezo yalizidi hata inashindikana kuyaeleza. Walikimbia huku na huko katika fadhaa yao na mahangaiko ya kushangaza. Katika shida iyo walikuwa wakilia na kusema kuwa “Mwisho wa ulimwengu umekuja” Akina mama walikimbilia wakilia huku wamewasahau watoto wao, wakizikumbatia sanamu zao za kusulubishwa kwa Yesu. Wengi walikimbilia makanisani wakitafuta wongofu, lakini ilikuwa kazi bure. Walikimbia madhabahuni, wakikumbatia sanamu zao, lakini wote, mapadri na watu wengine walifunikwa na uangamivu katika tetemeko hiloTU 143.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents