Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mwezi Kama Damu

  Wala giza la usiku lilikuwa silo la kawaida, na la kutisha kama la mchana. Walakini lilikuwa mbalamwezi pevu bila kitu cha kuiziba. Lakini weusi uliukuwa mzito, ambao kama mwanga wa mshumaa au taa, ukionekana katika nyumba za jirani au mahali pengine mbali kidogo, ilionekana kama giza la Misri lisilopenyeka kwa nuru. Kama kila mtu angekuwa amefunikwa na kitu kisichopeneyeka kwa nuru, hata hivyo giza lisingekamilika kwa jinsi lilivyokuwa kubwa. Baada ya usiku wa manane giza lilitoweka, na mwezi mara ya kwanza ukaonekana kama damu.TU 144.5

  Mei 19, 1780 unajulikana kihistoria kama, “Siku ya Giza” Tangu wakati wa Musa hakuna giza lililolinganishwa na hilo lililotokea. Maelezo ya shahidi aliyeshuhudia giza hilo ni mwangwi wa yale yaliyomo katika Yoeli yaliyoandikwa zamani za miaka 250 kabla nayo husema “Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla haijaja hiyo siku ya Bwana iliyo kuu na itishayo” Yoel 2:31.TU 145.1

  Kristo alisema, “Basi haya yaanzapo kutokea, changamkeni, mkaviinue vichwa vyenu, kwa kuwa ukombozi wenu umekaribia Wakati iishapo kuchipuka, mwaona na kutambua wenyewe ya kwamba majira ya mavuno yamekwisha kuwa karibu. Nanyi kadhalika, mwonapo mambo hayo yaanzapo kutokea, tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu u karibu”. Luka 21:28, 30-31.TU 145.2

  Lakini upendo wa Kristo na imani ya kuja kwake vimepoa kanisani. Watu wa Mungu walikuwa vipofu, wasizitambue dalili za kuja kwake, wala mafundisho ya Mwokozi kuhusu dalili hizo. Fundisho la kurudi kake Yesu halikujaliwa, mpaka baadaye likasahauliwa, hasa huko Marekani. Shughuli za uchumi na kutafuta mafanikio heshima zimewasahaulisha watu wasielewe kuwa mambo ya sasa yatapita.TU 145.3

  Mwokozi alitaja hali ya uasi itakayoonekana duniani kabla ya kuja kwake mara ya pili. Kwa watu wale wanaoishi wakati huu, Kristo anawaonya akisema “Basi jiangalieni mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafla, kama mtego unasavyo”. “Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu” Luka 21: 34,36. Ilikuwako haja ya lazima ya kuwaamsha watu wajiandae kukabili mambo yanayoambatana na kufungwa kwa muda wa rehemaTU 145.4

  “Kwa kuwa siku ya Bwana ni kuu, yenye kitisho sana naye ni nani awezaye kusimama?” Nani atasimama mbele yake Mwenye “Macho safi” yasiyotazama ukaidi na uovu? “Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi, nami nitayaangusha chini majivuno yao makali” “Falme yao wala adhabu zao havitaweza kuwaokoa” “Na huo utajiri wao utakuwa mateka na yumba zao zitakuwa ukiwa” Yoel 2:11; habakuki 1:13; Isaya 13:11; Sefania 1:18;13.TU 145.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents