Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Miller Apata Rafiki

  Miller asema, “Kwa ghafla tabia ya mwokozi ikajidhihirisha katika moyo wangu na katika nia yangu. Ilionekana kwamba, kulikuwa na wema wa huruma kwake, kiasi cha kumsukuma ajitoe kwa ajili yetu ili tuokoke na adhabu ya dhambi. Sasa swali ni kuwa, Inathibitikaje kuwa mtu wa namna hiyo yuko? Bila kupata habari hizo katika Biblia, hakuna pengine pa kuthibitishia. Mwokozi wa aina hiyo aelezeki kwingineko, ila katika Biblia.”TU 151.1

  Nikaona kuwa Biblia ndiyo inatoa maelezo dhahiri kuhusu kitabu ambacho hakikuandikwa kwa uongozi wa Mungu kinawezaje kuonyesha njia sahihi kwa ajili ya walimwengu walioanguka dhambini. Ni lazima Biblia kiwe ndicho kitabu cha Mungu. Basi Biblia kikawa ndicho kitu nilichokipenda na katika Yesu nikapata starehe kamili. Ndiye rafiki wa kweli. Basi Yesu akawa ndiye mpenzi wangu, miongoni mwa elfu kumi. Biblia ambayo kabla ya hapo ilikuwa giza sasa ikaniwia taa ya miguu yangu. Nikaona kuwa Mungu ndiye mwamba katika mawimbi ya maisha. Biblia ikiwa ndilo somo langu. Nikashangaa kwa kutoona thamani yake hao mwanzoni. Sikupenda kusoma kitabu kingine, na kupata hekima ya Mungu katika Biblia.TU 151.2

  Miller akaiungama imani yake dhahiri. Lakini wakafiri ambao walikuwa wenzake walimbishia yote aliyokuwa anawaeleza sana. Akaazimu kujifunza na kuhakikisha kuwa sehemu zile alizodhani kuwa hazikubaliani, sivyo ilivyo.TU 151.3

  Akitumia Commentary, alichunguza fungu kwa fungu na kulinganisha fungu na fungu, na kutumia vitabu vingine, kama Concordance akaanzia tangu Mwanzo, akisoma fungu kwa fungu na kulinganisha, alipoona kuwa hakuna mafarakano, basi alikaza mafundisho yake kwa ukamilifu, akilinganisha fungu na fungu. Ndipo akaona yale Daudi aliyoona katika Zaburi 119:130: “Kufafanusha maneno yako kwatia nuru na kumfahamisha mjinga”.TU 151.4

  Kwa juhudi nyingi, huku akifurahiwa sana, Miller alijifunza unabii wa Daniel na Ufunuo na kuona kuwa mifano, iliyotumiwa katika vitabu hivyo inaweza kufahamika, ingawa ni ya unabii. Akaona kwamba inaweza kujieleza na kufahamika, au kuelezwa na mafungu mengine. Juhudi yake ikampatia ujuzi halisi. Akafuatia unabii hatua kwa hatua, Malaika wa mbinguni walikuwa wakimwongoza.TU 152.1

  Alitosheka kuwa, mawazo ya watu juu ya miaka elfu ya muda kabla mwisho wa dunia, hayaungwi mkono na Neno la Mungu. Mawazo haya yanayosema kuwa kutakuwa na muda wa starehe ya miaka elfu kabla Kristo hajaja, ni kinyume cha mafundisho ya Kristo na mitume wake, ambayo husema, ngano na magugu yatakuwa pamoja mpaka wakati wa mwisho, na kwamba waovu watazidi kuwa waovu tu. 2Timotheo 3:13.TU 152.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents