Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Uasherati wa Kiroho

  “Kutokuwa mwaminifu kwa Kristo, kanisa hukaribisha mambo machafu ya ulimwengu yaliingilie, ambavyo hufananishwa na uasherati unaovuruga ndoa safi. Dhambi ya Israeli ya kujitenga na Bwana, hufananishwa na jambo hili. Hakika kama vile mke amwachavyo mumewe kwa hiana, ndivyo mlivyonitenda mimi kwa hiana, Ee nyumba ya Israeli, asema Bwana”, “Mke wa mtu aziniye! Akaribishaye wageni badala ya mumewe” Eze. 16:32. Yer. 3:20.TU 183.1

  Mtume Yakobo asema, “Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu Basi kila anayetaka kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu”. Yakobo 4:4.TU 183.2

  Mwanamke (Babeli) alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake ….. Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, “BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI” Nabii alisema, “Nikamwona mwanamke yule amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu”. Babeli ni Mji ule mkubwa “wenye ufalme juu ya wafalme wa nchi” Ufunuo 17:4-6, 18.TU 183.3

  Uwezo uliokuwa ukitawala Wafalme na Wakuu wa jamii za wakristo kwa karne nyingi ni Rumi. Mapambo ya rangi mbalimbali na dhahabu na lulu yote yalikuwa ya Rumi. Hakuna uwezo mwingine wowote ambao unaweza kulingana na elezo lisemalo, “umelewa kwa damu za watakatifu” kama kanisa lililowatesa watu wa Mungu yaani Rumi.TU 183.4

  Babeli pia imelaumiwa kama kuungana na wafalme wa nchi. Kanisa la Kiyahudi kwa kule kujiunga na mataifa makafiri na kujitenga na Mungu likawa kahaba. Rumi nayo kule kutafuta msaada kwa serikali ili kuendesha mambo ya kanisa, lilipata lawama ile ile.TU 184.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents