Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ujumbe Ulitolewa Kwa Wakati Hasa.

  Hali kadhalika Miller na wenzake walitimiza unabii, wakatoa ujumbe ambao ulitabiriwa kuwa utatolewa ulimwenguni. Kama wangalitambua kuwa wakiutoa utawaletea uchungu wasingeutoa. Ujumbe wa malaika wa kwanza na wa pili ulitolewa kwa wakati wake hasa, na ukatimiza kusudi la Mungu.TU 193.3

  Ulimwengu ulikuwa ukitazamia kuwa kama Kristo hataonekana, hali ya marejeo ingeachwa, yaani kanisa la marejeo lingetupwa. Lakini kwa kuwa wengi walitupa imani yao kulikuwako na wengine waliosimama imara. Matunda ya marejeo, roho ya kujichunguza, na kuukana ulimwenguni, huthibitisha kuwa ilikuwa kazi ya Mungu. Hawakuthubutu kukana kuwa Roho Mtakatifu hakuwaongoza waliohubiri ujumbe wa malaika wa pili. Wala hawakupata kasoro yo yote kama unabii na nyakati zilizosemwa. Wapinzani wao hawakuweza kukanusa tafsiri ya unabii, jinsi walivyoueleza. Hawakuweza kukanusha hali ya kiroho iliyokuwako kwa maombi ya bidii na kuchunguza Maandiko kwa bidii ili kuweza kuwapinga wapinzani wote walio hodari.TU 193.4

  Watu wa marejeo, yaani Waadventista waliamini kuwa Mungu alikuwa amewaongoza ili kutoa maonyo ulimwenguni, kuhusu saa ya hukumu. Wasema, Ujumbe huu umewajaribu wote waliousikia kwamba wale wote watakaojichunguza mioyo yao watafahamu upande wanaosimama ….. “watakapokuwa wamekutwa, kama Bwana angekuja” …. Sijui kama wangeweza kusimama na kusema, “Huyu ndiye Bwana wetu, tumemngojea, atuokoe au wangelikimbia uso wake wakiita miamba iwaangukie ili kuwafunika wasiouone uso wake aketiye juu ya kiti cha enzi”.TU 194.1

  Hali ya watu ambao bado wanaamini kuwa Mungu bado anaongoza wanaelezwa kwa usemi wa Miller: “Tumaini langu la kurudi kwake Bwana linasimama imara kama hapo mwanzo. Nimetenda yote kama nilivyoona kuwa ni wajibu kutenda, baada ya miaka ya kutafakari” “Maelfu mengi ya watu wamejifunza na kuhubiri kuhusu wakati, na kwa damu ya Yesu wamepatanishwa na Mungu”.TU 194.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents