Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Siri ya Hema Takatifu Yadhihirika

  “Hema takatifu” ya kweli iliyoko mbinguni, ndiyo hema takatifu ya agano jipya. Kristo alipokufa huduma ambazo zilikuwa kivuli tu, zilikoma. Wakati Daniel 8:14 ilipotimizwa kama ilivyoamuriwa, patakatifu panapotajwa lazima pawe pale pahusupo agano jipya. Hivyo basi unabi unaposema “hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa” huzungumzia patakatifu pa mbinguni.TU 200.1

  Lakini kutakaswa kwa patakatifu humaanisha nini? Je, inawezekana kuwa ni kitu mbinguni kinachohitajika kutakaswa? Katika Waebrania 9 utakaso wa patakatifu na duniani na pa mbinguni kumeelezwa dhahiri. “Na katika Torati karibu vitu vyote husafirishwa kwa damu, na pasipo damu hakuna ondoleo. Basi ilikuwa sharti nakala za mambo yaliyo mbinguni zisafishwe kwa hizo(damu za wanyama); lakini mambo ya mbinguni yenyewe yasafishwe kwa dhabihu zilizo bora kuliko hizo.” Waebrania 9:22-23, yaani damu ya thamani ya Kristo.TU 200.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents