Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Siku Za Hatari Kwa Kanisa

  Watu waaminifu walioshikilia ukweli walikuwa wachache. Wakati fulani ilionekana kana kwamba ubaya utatawala na kufunika ukweli kabisa. Kiasi cha kutoweka nchini. Injili ilitoweka na watu walishikilia tu mambo yaliyoshurutishwa kufanya. Walifundishwa kutegemea matendo yao mema ili kuwatakasa, na kuwaondolea dhambi. Waliambiwa mambo mengi sana yawezayo kuwapatanisha na Mungu na kuwapa haki ya kuwa watakatifu mbele za Mungu. Baadhi ya mambo hayo ni: kwenda safari ndefu za kuhiji, kulipa kitubio, kuabudu watakatifu kujenga makanisa, mahali patakatifu, madhabahu, kutoa mali nyingi kanisani. Mambo hayo yangewaletea upendeleo mbele za Mungu.TU 17.4

  Panapo mwisho wa karne ya nane, wafuasi wa kanisa la Rumi (Roma Catholic) walidai kwamba kwenye karne za mwisho wa kanisa askofu wa Rumi alikuwa na uwezo katika mambo ya kiroho ambao unaonekana siku hizi. Maandiko ya kwanza yalikosewa na watawa. Maamuzi ya mabaraza ambayo yalikuwa hayajasikiwa yaligunduliwa, nayo yanamwezesha Papa kuwa na madaraka makuu ulimwenguni pote. Maamuzi haya ni ya mwanzoni kabisa.TU 17.5

  Waaminifu wachache ambao wanasimama katika msingi wa kweli (Kor. 3:10-11) walitatanika. Wakiwa wamechoshwa na mapambano ya daima juu ya kweli na uongo, na mateso yasiyokoma na matatizo ya kila aina ambayo shetani amewaletea, baadhi yao walikata tamaa. Kwa ajili ya kuhofia maisha yao na mali zao, waliacha unyofu wao, wakaondoka katika msingi wa kweli. Wengine walikuwa majasiri katika kupingana na adui zao.TU 18.1

  Ibada ya sanamu ilienea pote. Mishumaa iliwashwa mbele ya sanamu, na watu walizifanyia ibada na maombi. Matendo ya kipumbavu yalienea kuhusu dini. Watu wakajifanyia mambo tu bila kufikiri. Wakati huo huo, maaskofu na makasisi walikuwa wametopea katika anasa na ufedhuli, ambavyo watu waliwatazamia katika kuwaongoza. Hivyo watu wakafungwa katika ujinga na ubaradhuli.TU 18.2

  Katika karne ya kumi na moja, Papa Greory VII alidai kuwa kanisa kamwe halijakosa hata kidogo wala halitakosa kamwe kama maandiko yasemavyo. Lakini maandiko hayadhibitishi madai hayo. Hata papa wa Rumi mwenye majivuno pia adai kuwa anao uwezo wa kuwaondoa wafalme katika utawala. Kithibitisho cha majivuno hayo kilikuwa kivitendo kilichotendwa kwa mfalme wa ujerumani, Henry IV. Kwa kuwa hakujali Papa, alizuiliwa na kutolewa katika utawala kwa njia ya amri ya papa kuwaamuru watoto wake mwenyewe wamwasi.TU 18.3

  Henry aliona kuwa ni lazima akaungame kwa Papa. Aliondoka Ujerumani yeye na mkewe na mtumishi wake mwaminifu wakasafiri kuvuka milima ya Alps wakati wa baridi, ili akajinyenyekeze mbele ya papa na kuomba msamaha. Alipofika kwa makao ya papa Gregory aliwekwa nje kwenye ukumbi wa baridi, pale akiwa hana kitu cha kujifunika baridi na akiwa hana viatu alisubiri papa amruhusu kufika mbele yake, huko ndani. Alingoja pale siku tatu huku akiomba na kuungama, ndipo aliporuhusiwa kuingia ndani. Hata hivyo aliruhusiwa kutawala kwa masharti. Hivyo papa Gregory alijisifu kuwa anao uwezo wa kuweka na kuondoa kiburi cha wafalme.TU 18.4

  Kuna tofauti kubwa kiasi gani baina ya mjivunaji huyu na Kristo. Yeye anayejieleza mwenyewe kuwa anasimama mlangoni akingojea kuingia. Kristo alifundisha kwamba: “Yeyote atakayekuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu”. Mathayo 20:27.TU 18.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents