Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kumngojea Bwana Wao.

  Lile tangazo kwamba, “Haya bwana arusi yuaja, liliongoza watu maelfu kukutazamia kuja kwa Bwana mara moja. Wakati ulipofika Bwana arusi alikuja, lakini sio duniani, bali alifika kwa Mzee wa siku huko mbinguni, katika karamu ya arusi, katika karibisho la ufalme wake. Wale waliokuwa tayari waliingia pamoja naye arusini. Hawakuweza kufika katika mwili, maana wao wako duniani. Wafuasi wa Kristo lazima wamngojee Bwana wao, mpaka atakaporudi kutoka katika arusi.” Luka 12:36. Lakini ni lazima wafahamu kazi yake, na kumfuata kwa kiroho katika imani. Kwa njia hii husema kuwa wanaingia arusini.TU 206.1

  Katika mfano, wale waliokuwa na mafuta katika taa zao waliingia arusini. Wale waliovumilia katika giza kuu na uchungu, wakingojea nuru zaidi huku wakichunguza Maandiko, walielewa fundisho la patakatifu pa mbinguni, na huduma Kristo aliyochukua. Walimfuata kwa imani katika kazi anayofanya katika patakatifu pa mbinguni. Na wote watakaopokea ukweli wa namna hiyo wakimfuata Kristo kiroho katika imani jinsi anavyofanya kazi yake ya uombezi, huingia arusini.TU 206.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents