Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Jinsi Mafundisho ya Uongo Yalivyoingia.

  Hata kabla ya kuingia upapa kanisani mafundisho ya kimizimu yalionekana kupokewa kanisani. Watu wengi walikuwa na hali ya mwenendo wa kimizimu, eti wapate kuwavuta wapagani kuingia kanisani. Kwa njia hiyo makosa mabaya sana yaliingizwa kanisani.TU 19.1

  Jambo kuu kati ya mafundisho haya ya uongo ni imani kwamba mtu anayo hali ya kutokufa, na kwamba mtu akifa roho yake haifi. Fundisho hilo ndilo lilikuwa msingi wa kanisa la Rumi kuimarisha sala ya wafu, na kumtumaini bikira Maria apate kuwaombea, Kutokana na hapo uzushi ukaibuka kwamba kuna moto wa milele utakaowateketeza waovu bila kuzimika.TU 19.2

  Njia ikafunguliwa ya kuingiza uzushi mwingine, kwamba huko ahera kuna mahali pa kutakasia dhambi (purgatory) ambao ni imani ya wamizimu, inayotumika kuwatishia watu na kuwashikilia katika hali ya ushirikina. Uzushi wa aina hiyo hudai kuwako huko ahera kuna mahali pa mateso makali ambayo watu wanaokufa hupitishwa humo kwanza mpaka watakaswe dhambi zao, ndipo huruhusiwa kuingia mbinguni.TU 19.3

  Kuna jambo jingine ambalo Rumi hulitumia ili kuzidi kuwaogofya wafuasi wake, nalo ni fundisho juu ya kusamehe dhambi. Msamaha kamili wa dhambi uliahidiwa kwa wote ambao wangejiunga na papa katika vita vyake na adui zake, kwa njia ya kulipa fedha kanisa, ambazo fedha za msamaha wa dhambi zote za zamani, na za sasa na zijazo. Basi walimwaga pesa ili kusamehewa dhambi, na kuwaondoa rafiki na jamaa zao waliokufa ambao wamo katika shimo la mateso. Kwa hiyo Rumi kajaza masanduku na pesa, ambayo ziliwawezesha kuishi kifahari, na huku wakijidai kuwa wanamwakilisha yule ambaye hakuwa na mahali hata pa kulaza kichwa chake.TU 19.4

  Huduma ya meza ya Bwana iliondolewa, badala yake akawekwa huduma ya kimizimu, yaani misa (mass). Makuhani wa papa wanajidai kuwa hugeuza ule mkate na ile divai kuwa “mwili na damu ya Kristo halisi”. Kwa kufuru nyingi hujidai kwa kiburi kuwa wanao uwezo wa kumwumba Mungu na kumgeuza mkate na damu kuwa Mungu, ambaye ni Mwumbaji wa vitu vyote. Wakristo walilazimishwa kuinama na kutenda mambo hayo, kwamba ndiyo ibada ya mbinguni.TU 19.5

  Katika karne ya kumi na tatu lilianzishwa jambo jingine la kutisha la kipapa ndilo baraza kuu la kuwahukumu wapingaji. Katika mabaraza yao ya siri, shetani na malaika zake ndio waliowaongoza waovu hawa. Malaika wa Mungu alisimama katikati bila kuonekana akiandika mambo yote, historia yao yote, na maamuzi yao ambayo ni ya kutisha. “Babeli mkuu amelewa kwa damu ya watakatifu” Ufunuo 17:5-6. Wafia dini mamilioni wanamlilia Mungu alipize kisasi kwa utawala huu mwasi.TU 20.1

  Utawala dhalimu wa kipapa umetawala dunia. Wafalme wa wafalme humwinamia Papa kwa muda wa miaka mamia mafundisho ya Roma yamepokewa sana. Waongozi wake wameheshimiwa na kukubaliwa. Kanisa la Rumi halijastawi na kufaulu kama sasa.TU 20.2

  Lakini, “adhuhuri ya upapa ilikuwa usiku wa manane wa ulimwengu”.TU 20.3

  Maandiko matakatifu hayakujulikana. Waongozi wa kiapa waliichukia nuru isije ikafichua dhambi zao. Sheria ya Mungu, ambayo ni kipimo cha haki, ilipokuwa imeondolewa, waliishi kifedhuli bila wasiwasi. Majumba ya akina papa na maaskofu yalijaa zinaa na ufedhuli, na ufasiki. Baadhi ya maaskofu walikuwa na hatia ya uasi na uvunjaji wa sheria kiasi cha kutovumiliwa na watawala wa Serikali. Kwa karne nyingi ulaya haikuwa na maendeleo katika elimu, na ustaarabu. Maendeleo ya elimu na ujuzi vimekufa ganzi katika mahali pa Ukristo.TU 20.4

  Hayo yamekuwa hivyo kwa sababu neno la Mungu lilipigwa marufuku.TU 20.5

  Marejeo: TU 20.6

  Cardinal Wiseman’s Lectures on “The Real Presence” Lecture 8, sec. 3 para 26. TU 20.7

  Wylie — History of Protestantism, Book 1, chapter4.TU 20.8

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents