Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  27/Uamsho wa Kisasa Unafauluje?

  Popote pale ambapo Neno la Mungu lilipohubiriwa kwa uaminifu matokeo yake yamethibitisha kuwa neno hilo ni la Mungu hakika. Wenye dhambi walijutishwa. Na toba ya kweli ilionekana kwao. Wakaufahamu utakatifu na haki ya Mungu jinsi ilivyo, kwa hiyo wakalia: “Ni nani ataniokoa na mwili huu wa mauti?” Warumi 7:24 Msalaba ulipoelezwa wazi wao walijiona kuwa si kitu ila huruma za Kristo na neema yake ndiyo itawaokoa tu. Kwa damu ya Yesu tu watapata “msamaha wa dhambi zilizopita”. Warumi 3:25TU 223.1

  Watu hawa waliamini na kubatizwa, wakawa wakitembea katika upya wa uzima. Kwa imani ya Mwana wa Mungu wakawa wakifuata nyayo zake, na kudhihirisha tabia yake ulimwenguni. Wakawa wakijitakasa kama yeye alivyo mtakatifu. Mambo ambayo waliyapenda zamani, sasa wanayachukia na kuyaacha; na mambo ambayo hawakuyapenda zamani, sasa wanayapenda na kuyatenda. Kiburi kimegeuka kuwa unyenyekevu, kutakabiari upuuzi vinageuka kuwa utu mwema. Walevi wanakuwa watu sawa. “Wakristo wanatafuta urembo wa moyoni, sio mapambo ya nje, yaani kusuka nywele, na kujipamba kwa dhahabu na lulu, na kuvalia mavazi ya thamani, bali utu wa ndani …. Wenye thamani kuu, ndiyo roho nyenyekevu, tulivu, ipendezayo mbele za Mungu”. 1Pet. 3:3-4.TU 223.2

  Uamsho uliwahusu wenye dhambi, kwa njia ya kuwaita ili watubu. Matunda yalionekana, sio kwa kufurahi katika anasa, ila kwa kuwa watu wanastahili kuteswa kwa ajili ya Kristo. Watu waliona mabadiliko katika maisha yao hao walioliungama jina la Kristo. Hali kama hiyo ndiyo ilikuwa ikionekana kwa watu waliopata uamsho miaka ya zamani.TU 223.3

  Lakini uamsho wa kisasa unatofauti. Ni kweli kwamba watu hujidai kuwa wameongoka na wako washiriki wa kanisa wengi makanisani. Walakini matokeo yake hayaonekani kufanana na uongofu halisi unaoonyesha hali ya maisha ya kiroho ya kweli. Huwa hali ya msisimko tu ambao haudumu ila baada ya muda kitambo hufifia na kurudi hali ya kawaida.TU 223.4

  Uamsho wa kijumla jumla huwa ni msisimko tu kwa ajili ya jambo lililoletwa. Uamsho wa namna hiyo huwa hauna haja na mafundisho ya Biblia ambayo ndiyo kweli. Ibada yo yote isipokuwa na mambo ya kuburudisha na kuchangamsha, haiwapendezi kabisa; wala haiwavutii.TU 223.5

  Mwongofu ye yote, uhusiano wake na Mungu, na mambo ya ufalme wa mbinguni, ndicho kitu kikuu katika maisha yake. Katika makanisa ya washiriki wengi iko wapi roho ya uwakfu wa kweli? Waumini hawakichukii kiburi na upendo wa anasa za ulimwengu.. Hawako tayari kujinyima na kujitoa wakfu. Wala hawako tayari kujikana nafsi, na kufuata unyenyekevu wa Kristo. Utauwa umetoka katika makanisa mengi.TU 224.1

  Ijapokuwa hali ya kuanguka kiimani imeenea makanisani, walakini kuna wafuasi wa kweli wengi katika makanisa haya. Kabla ya kuleta hukumu ya mwisho ya Mungu, kutakuwa na mwamko mkubwa katika watu wa Mungu ambao haujaonekana tangu siku za mitume. Roho wa Mungu atamwagwa. Watu wengi wataondoka katika makanisa hayo ambayo yanaongozwa na roho ya ulimwengu, na badala ya kumpenda Mungu na Neno lake. Wachungaji wengi wa watu wengi wataupokea ujumbe wa kweli kwa furaha, nao watajiandaa ili kumlaki Bwana arudipo.TU 224.2

  Adui wa wanadamu anatamani kuizuia kazi hii, atafanya hivyo kwa njia ya kuinua kundi la kuigiza. Ataigiza uongofu, kana kwamba Mungu amewamwagia Roho Mtakatifu. Atafanya hivyo katika makanisa yatakayompa nafasi hiyo. Watu wengi watajipa kwamba Mungu anatenda maajabu, kumbe kazi hiyo hutendwa na watu wenye roho tofauti na Roho wa Mungu. Shetani atataka kuendeza mvuto wake kwa wakristo, kwa njia ya kujifanya kuigiza kazi ya kanisa la Mungu. Ataigiza kazi ya Mungu ili apotoshe watu. Basi patakuwa na msisimko mkubwa wenye mchangayiko wa ukweli na uongo, ili apate kuwakosesha watu.TU 224.3

  Lakini kwa nuru ya neno la Mungu, watu hawa watatambulikana kuwa ni wa aina gani. Popote watu wanapopuuza uthibitisho wa Neno la Mungu, na kugeukia mambo mengine tutakuwa na hakika kuwa Mungu hayumo kati yao. Jambo ni kwamba: “Mtawatambua kwa matunda yao” Mathayo 7:16. Hicho ndicho kipimo kwamba hawa sio wanaoongozwa na roho wa Mungu.TU 224.4

  Ukweli wa neno la Mungu ni ngao ya kuyapinga madanganyifu ya Shetani. Kutojali ukweli huu kumfungulia Shetani apate kuingiza maovu ya kila namna ulimwenguni. Sheria ya Mungu haikujaliwa kabisa. Makosa katika kueleza toba na utakaso yameingia yaliyoleta udanganyifu mwingi, ukawafanya watu washushe kipimo cha Ukristo. Hapa ndipo siri ilipo ya upungufu wa Roho wa Mungu katika uamsho wa siku hizi.TU 224.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents