Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Sheria ya Uhuru.

  Walimu wengi wa dini hudai kuwa Kristo alipokufa msalabani aliiondoa sheria. Wengine huiita kongwa ya utumwa, kwa hiyo hudai uhuru wa dini, katika furaha ya Injili.TU 225.1

  Lakini manabii na mitume hawakudai jinsi hiyo kuhusu sheria takatifu ya Mungu. Daudi alisema, “Nami nitakwenda panapo nafasi kwa kuwa nimejifunza mausia yako”. Zab. 119:45. Mtume Yakobo asema kuhusu amri za Mungu, “Sheria kamilifu ya uhuru” Yakobo 1:25. Mwandishi wa ufunuo hutaja mibaraka kwa mtu yule “ashikaye amri, awe na ruhusa ya kuuendea mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake”. Ufunuo 22:14.TU 225.2

  Kama ingewezekana kuwa sheria ifutwe au ibadilishwe, Kristo asingelikufa ili kumwokoa mwanadamu atoke katika adhabu ya dhambi ya kuvunja sheria. Mwana wa Mungu alikuja ili kuitukuza sheria na kuifanya iheshimiwe, Isaya 42:21, alisema, “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati” …. Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka Kumhusu yeye mwenyewe, alisema, “Kuyafanya mapenzi yako, Ee, Mungu wangu, ndiyo furaha yangu; Naam, sheria yako imo moyoni mwangu” Mathayo 5:17-18; Zaburi 40:8.TU 225.3

  Sheria ya Mungu haibadiliki ni ufunuo wa tabia ya Mtoaji wake. Mungu ni pendo na sheria yake ni pendo. “Pendo ni utimilifu wa sheria” Mtunga Zaburi asema, “Sheria yako ni kweli” “Maagizo yako yote ni ya kweli” Paulo asema, “Torati ni takatifu na ile amri ni takatifu, na ya haki na njema,” Warumi 13:10; Zaburi 119; 142, 172; Warumi 7:12. Sheria kama hiyo inadumu sawasawa na mwenye kuitoa anavyodumu.TU 225.4

  Ni kazi ya kuongoka kwa kweli na kutakaswa ndiyo inayoleta upatanisho na Mungu; na kuwaleta wanadamu wapatane na sheria yake. Hapo mwanzo mtu alikuwa katika umoja kamili na Mungu wake, na sheria yake. Lakini dhambi ilimfarakanisha na Mwumbaji wake. Moyo wake daima ukawa haupatani na sheria ya Mungu. Na ya mwili ni uadui juu ya Mungu, “kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii” Warumi 7:8. Lakini “Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee” ili mtu apatanishwe na Mungu na kurudishiwa uhusiano na Muumba wake. Badiliko hili ndilo kuzaliwa kupya, na ambako lisipopatikana mtu hawezi kuuona ufalme wa Mungu Yohana 3:16.TU 225.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents